Na Theophilida Felician Kagera.


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan amefanya uzinduzi wa chuo cha mafunzo stadi VETA Burugo kilichojengwa Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera.

Rais Samia akiwa chuoni hapo Leo hii kwa ajili ya zoezi la uzinduzi wa chuo hicho amefafanua  kuwa  kutokana na juhudi kubwa zilizotumika katika ujenzi  wake haina budi  watu wote  kwa pamoja  kukitunza vyema ili kipate kudumu na kuwasaidia vijana wote watakaohitaji chukuwa kozi za  mafunzo stadi mbalimbali yatakayo kuwa yakifundishwa katika chuo hicho.

Chuo hicho kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh Bilioni (22) kwa hisani ya Serikali ya China kina jumla ya Madarasa (218) kina uwezo wa kuchukuwa wanafunzi  Elfu (1000) wa kozi za muda mfupi na wanafunzi  mianne (400) wa kozi za muda murefu.

Pia kina ofisi nane( 8) za walimu, nyumba za walimu (3) bweni lenye uwezo wakuchukuwa wanafunzi  (214) wakike na (116) wakiume. 

Hata hivyo ameongeza kuwaelezea wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo la chuo hicho ya kwamba Serikali inaendelea na mbio zaidi katika kuhakikisha inaboresha mazingira ya elimu hapa nchini lengo ikiwa ni kutaka kuwasaidia vijana wakitanzania  ili wanufaike kielimu, kiujuzi na kadharika.

Sambamba na hayo amesema atawalipia ada wanafunzi wa kike (20) wakiume (10) na wengine (10) watakokuwa wakitokea katika familia duni ili wapate kusoma vyema katika chuo hicho kilichojengwa kwa kiwango cha hali ya juu mno.

Share To:

Post A Comment: