Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Iringa SF Isabela Mbwago amethibisha kutokea kwa ajali ya moto katika Mji wa Mafinga Jambo ambalo limewasababishia hasara wafanyabiashara wa eneo hilo

Kamanda SF Mbwago ameeleza sababu za kutokea kwa moto huo sanjari na kuwasihi wananchi kuendelea kufuata taratibu zote za ujenzi ikiwemo kupata ushauri wa ujenzi salama wa majengo

Alisema kuwa Moto huo uliozuka usiku wa saa saba kuamkia leo Oktoba 21,2022 Mjini Mafinga umeteketeza vibanda 15 vya  wafanyabiashara eneo la kwa Ben Studio. 

Kwa upande wake Shuhuda wa tukio la moto huo ambaye ndiye mmiliki wa jengo hilo bwana Mohamed Migira amesema moto huo ulianza majira ya saa saba za usiku na baada ya hapo alitoa taarifa kwa jeshi la zimamoto lakini jitihada zake hazikufua dafu.

Penina Kidumage ni mmoja wa wahanga waliopotelewa mali zao kutokana na ajali hiyo ya moto yeye anasema alipigiwa simu na baada ya kufika eneo la tukio aliishia kuuangalia moto ukiteketeza mali zake kwani hakuwa na uwezo wa kuuzima.

Share To:

Post A Comment: