Kwa maisha yetu hususani mijini ni vigumu kulima mbogamboga nyumbani hivyo tumekua tukitegemea mboga za kununua ambazo mara nyingine zimekua si salama kwa matumizi ya binadamu kutokana na maeneo zinapolimwa hata maji yanayotumika kumwagilia.
Sasa kuna uwezekano wa mwenyewe kulima mbogamboga nyumbani kwako. Acha visingizo kwani inawezekana kuwa mkulima wa mbogamboga mwenyewe nyumbani kwako kwa kutumia ndoo ambazo hazitumiki tena, mabeseni hata vyungu ambavyo hutumika kupanda maua. 
Leo tuangalie baadhi ya mboga ambazo unaweza kuzipanda mwenyewe nyumbani na jinsi ya kuzipanda.
KAROTI
Watu wengi tunaifahamu karoti kama kiungo kwenye mapishi tofauti tofauti na pia kama mboga, karoti ni moja ya mbogamboga unazoweza kulima kwa kutumia makopo.

Jinsi ya kupanda:
chagua kopo ambalo ni refu kwenda chini, Tafuta udongo wenye rutuba ambao hauna mawe, inafaa zaidi udongo wa kununua kwa sababu udongo wa kuchukua popote huwa hauna rutuba ya kutosha na huwa unavimelea vya kuua mmea.

kwa kila kopo moja panda karoti moja kwa mbegu au mche wa karoti. Usitie mbolea kwenye udongo kabla ya kupanda mbegu.

Ukipanda jitahidi kumwagilia mara kwa mara usiache udongo ukauke kabisa mwagilia angalau mara moja kwa wiki maana maji mengi yataozesha mizizi
Weka mbolea kuanzia wiki ya 5-6 baada ya kupanda.Karoti zitakua tayari kuvunwa baada ya miezi miwili na nusu au vile utakavyopendelea ziwe kulingana na matumizi yako.

BIRINGANYA
Ni mboga inayovutia sana kwa rangi hata muonekano.

Jinsi ya kupanda:

Chukua makopo yako au vyungu kulingana na idadi unayotaka kupanda
Panda mbegu ya biringanya moja au mbili kwa kila kopo.Mwagilia vizuri na weka mbolea kila baada ya wiki mbili. Unaweza kuvuna baada ya 16 mpaka 24 baada ya kupanda baada ya kuona ngozi ya nje inang’aa na haina mikunjo.

NYANYA

Jinsi ya kupanda
• Kwa kutumia makopo yako weka udongo kwa kila kopo.
• Baada ya kuweka udongo changanya na mbolea vizuri
• Kwa kila kopo moja panda mche moja wa nyanya au mbegu
• Mwagilia vizuri baada ya kupanda miche yako kwa mfululizo siku za kwanza na endelea kumwagilia miche mpaka itakapokua
• Weka mbolea tena wiki mbili kabla ya kuvuna nyanya zako
• Acha nyanya zako mpaka zikomae na unaweza kuvuna utakapoona nyanya imeiva na kuwa nyekundu kabisa haijalishi saizi itakayokua nayo.
Hayo ni baadhi ya mazao ambayo unaweza kulima kwa kutumia makopo nyumbani ila yapo mengi sana hivyo ni wajibu wako kuhakikisha unajikita kwa kufanya kilimo cha aina hii acha kusingizia ya kwamba huna eneo.
Share To:

Post A Comment: