karoti inarutubisha cells mwilini na kuzifanya zisizeeke haraka. Hii inatokana na uwepo wa Vitamin A ambayo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa macho kuona.

Karoti husaidia kuondoa sumu na taka mwilini, inaondoa mafuta yasiyotakiwa katika ini (Cholesterol) na kuliwezesha lifanye kazi vizuri, kusafisha njia ya haja kubwa na kusaidia kupata choo vizuri (kuzuia constipation).

karoti hupunguza hatari ya kupata SHINIKIZO LA DAMU (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (blood vessels) na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).

karoti husaidia kuimarisha macho kuona vizuri, mfano tatizo la kutoona vizuri usiku, pia inasaidia kuondoa matatizo ya allergy kwenye macho mfano macho kuwasha sababu ya vumbi.

Karoti zinasaidia kufanya fizi na meno kuwa imara na kuchochea uzalishwaji wa mate.

Pia inasaidia kuzuia stroke(Kiharusi), Watafiti wa Harvard University wamegundua kuwa watu wanaokula karoti walau sita kwa wiki wana uwezekano mdogo wa kupata stroke.
Share To:

Post A Comment: