Na Dotto Kwilasa, DODOMA

HOSPITAL ya Benjamin Mkapa (BHM) imefanikiwa kupandikiza figo kwa watu 31 na kuokoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi billion 2.3 huku ikitibu watu 715 ugonjwa wa Moyo na kati yao 39 walibainika na matatizo ya moyo nakuwekewa vipandikizi na kati yao 8 wamepandikiziwa betri kwenye moyo.

Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya hospitali hiyo na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023, Dkt. Alphonce Chandika mkurugenzi mtendaji hospital hiyo (BHM) amesema watoto 14 waliozaliwa na shida ya moyo wametibiwa huku watoto 10 wakifunguliwa vifua na kufanyiwa upasuaji.

Amesema bilioni 1.28 zimeokolewa kwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa 58 wa nyonga kwakuwawekea vipandikizi kwa gharama ya shilingi milioni 12 badala ya kutibiwa nje ya nchi kwakiasi cha shilingi milioni 35 kwa mgonjwa mmoja.

katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema BMH imeanza kutoa mafunzo kwa wataalamu wa usingizi na ganzi na tayari wataalamu 127 wamehitimu huku akibainisha kuwa hospiltal hiyo inakwenda kuongeza wigo wa huduma kwakujenga jengo maalum kwaajili ya matibabu ya moyo, upasuaji wa mifupa na ubongo ili  kuhakikisha hospital hiyo inakuwa ya pili ya taifa.

Hospital ya Benjamin Mkapa ilijengwa kwa dhamira kuu ya kutoa matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi ili kutibu magonjwa ambayo yamekuwa hayatibiwi hapa nchini.

Share To:

Post A Comment: