Na John Walter-

Manyara Serikali imesema ipo makini kuwahudumia watu wote wakiwemo wenye ulemavu ambapo imeandaa miundombinu rafiki katika ofisi zote za serikali kuwawezesha wenye ulemavu kupita na kupata huduma.

Hayo yameelezwa Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) aliyemwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa, Patrobas Katambi katika kilele cha Maadhimisho ya fimbo nyeupe yaliyofanyika kitaifa mkoani Manyara. 

Amesema katika kuwathamini watu wenye ulemavu, Serikali imeajiri walimu maalum kwa ajili ya kuwafundisha wenye mahitaji maalum. Aidha ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa kusimamia kikamilifu pesa zinazotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili ukawanufaishe wenye Ulemavu. 

 Akielezea maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe Mwenyekiti wa chama Cha Wasio ona Tanzania (TLB) Omari Sultan Mpondelwa, amesema ni jukwaa la wasio ona kukutana, kuweza kujieleza,kuielimisha jamii juu ya uwezo wao, na mahitaji yao katika nyanja zote za maisha. Mwenyekiti huyo wa TLB amesema Wapo watumishi wengine wametelekezwa na waajiri wao baada ya kupata shida ya kutokuona bila kupatiwa stahiki zao zinazohitajika huku wengine wakikosa mkataba licha ya shida hiyo kuipata wakiwa katika majukumu. 

Aidha amesema wanachohitaji wao katika jamii ni kuthaminiwa, kujumuishwa na kupewa taarifa mbalimbali juu ya kazi za serikali. Ameleza kuwa Uimara wa Chama cha watu Wasio ona unategemea nguvu ya wanachama wenyewe, serikali ambaye ni mlezi na wadau wengine wa Maendeleo. Kuhusu Changamoto walizonazo watu wenye ulemavu wa kuto kuona Mpondelwa amesema ni pamoja na Unyanyapaa, umaskini na nyingine nyingi ambazo bado serikali na wadau mablimbali wanaendelea kuwaunga mkono.

Amewataka watu Wasioona kujipambania wenyewe kutatua changamoto zao badala ya kusubiri msaada tu kutoka Kwa watu wengine. Mwenyekiti wa TLB amekiri kuwa baadhi ya watu wenye shida ya kutokuona wanasubiri kusaidiwa zaidi kuliko kujisaidia wao wenyewe jambo linalowafanya kuwa tegemezi. Serikali imesema ipo makini kuwahudumia watu wote wakiwemo wenye ulemavu ambapo imeandaa miundombinu rafiki katika ofisi zote za serikali kuwawezesha wenye ulemavu kupita na kupata huduma. 

"Serikali inawatambua wenye ulemavu na inajua kabisa hujafa hujaumbika hivyo unapotoa kwa ajili ya wenye ulemavu unaweka hazina mbele ya Mungu" Hayo yameelezwa na Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) aliyemwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa, Patrobas Katambi katika kilele cha Maadhimisho ya fimbo nyeupe yaliyofanyika kitaifa mkoani Manyara. Amesema katika kuwathamini watu wenye ulemavu, Serikali imeajiri walimu maalum kwa ajili ya kuwafundisha wenye mahitaji maalum. Aidha ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa kusimamia kikamilifu pesa zinazotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili ukawanufaishe wenye Ulemavu. 

 Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere ameipongeza kamati ya maandalizi kwa kushirikiana na kufanikisha zoezi hilo muhimu lilidimu kwa siku tatu likienda sambamba na kongamano la siku mbili lililofanyika ukumbi wa chuo kikuu Huria mjini Babati. Aidha TLB Wamependekeza mkoa unaofuata kuadhimisha Fimbo Nyeupe mwaka 2023 iwe mkoa wa Mara.
Share To:

Post A Comment: