DENIS CHAMBI, TANGA.

Bodi ya Filamu Tanzania leo mkoani Tanga imeanza zoezi la ukusanyaji wa kazi za sanaa  za wasanii wa  filamu mbalimbali   hapa nchini kwaajili ya kuzishindanisha kwenye kinyang'anyiro cha kushindania tuzo za filamu kwa mwaka huu wa 2022.

Akizungumza meneja mipango na masoko kutoka Bodi ya filamu Tanzania Goodluck Chuwa amesema kuwa wanaendelea  kuunga mkono juhudi za serikali kuzidi kuitangaza Tanzania kupitia filamu ikienda sambamba na uzinduzi wa royal tour ambayo ilizinduliwa   mwaka 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Meneja huyo alisema zoezi hilo la ukusanyaji wa filamu ambalo limezinduliwa  leo mkoani Tanga litaendelea hadi October 30 ambapo kazi za wasanii kutoka mikoa zaidi ya 18 zitakusanywa zikishindanishwa katika   vipengele  31.

"Mkoa wa Tanga umekuwa wa kwanza kabisa katika  kukusanya filamu hizi lengo ni kuhakikisha wasanii wa sekta ya filamu wanaendelea kunufaika  katika  Mapinduzi makubwa ambayo yanafanywa na serikali , tutakumbuka  Mheshimiwa Raisi alifanya filamu ya royal tour   hii ni kama taa inayotuambia kuwa  sekta ya filamu inakwenda kubadilika sio tu kwenda kupata Umaarufu lakini sasa hivi filamu ni biashara na uchumi , filamu ni kazi, tutapita zaidi ya mikoa 18 ya Tanzania bara na mwisho wa mwezi huu itakuwa ni mwisho wa kupokea filamu zote" alisema Goodluck.

Aidha ameipongeza serikali kwa kuanzisha mashindano hayo ya filamu ambayo yameleta mapinduzi makubwa na kuinua ari na hamasa  kwa wasanii mbalimbali hapa nchini ambapo sasa kazi zao zinaonekana na kuingia kwenye masoko ya kiushindani hadi nje ya nchi.

"Tulikuwa hatuna tuzo za filamu lakini bodi ya filamu ilianzisha mchakato huu ambao mpaka sasa umeleta mafanikio makubwa tumeshuhudia wenzetu sasa hivi kupitia sekta hii wameanza kunufaika tumeanza kuona washindi kwenye shindano la kwanza la mwaka jana lililofanywa na serikali na  Slsasa hivi tunaona filamu nyingi zinaingia kwenye masoko ya kimataifa"  alisema

Afisa utamaduni wa mkoa wa Tanga Emmanuel Makene amewataka wasanii wa filamu  kuendelea kupelekea kazi zao nyingi zitakazoingia kwenye ushindani na mikoa mingine na hatimaye kuufanya  mkoa huo kuibuka na ushindi.

"Tumefarijika sana na ujio wa bodi ya filamu Tanzania  tutaendelea kukusanya kazi zote za wasanii ambao wanatakiwa wazifikishe kwenye ofisi ya mkoa ya utamaduni lakini msanii kama unaweza  kwenda katika ofisi za makao makuu ya bodi ya filamu ukaziwasilisha wewe mwenyewe, rai yangu wasanii wajitokeze mapema ili mchakato huu ufanyike mapema kwa uhakika zaidi" alisema Makene.

Mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa Tanga Mohammed Amri Majuto  na mkurugenzi wa Majuto Sanaa group alisema amewataka wasanii kutumia fursa ya filamu kujiingizia kipato akiwataka wanatanga kuwapigia kura katika kinyang'anyiro hicho.

"Tunashukuru bodi ya filamu kutuletea fursa hii mkoa wa Tanga tupende sana kuzitumia kwa sababu zikishaondoka tutakuja kuzijutia na wasanii  hii ni nafasi yao kujitambulisha nina uhakika kwa filamu tulizoziandaa tutashinda katika vipengele mbalimbali tumejipanga vizuri na tumeandaa filamu  za kiushindani" alisema Majuto.

Baadhi ya wasanii waliokabidhi filamu zao akiwemo Haroun Mchuzi na Nasra Juma wameipongez bodi ya filamu kwa jitihada inazoendelea kuzifanya kuinua tahnia ya uingiaji hapa nchini huku wakieleza matumaini yao ya ushindi kwa kazi ambazo wameziwasilisha  na kuwataka wananchi wa mkoa wa Tanga pamoja na wadau wa filamu kujitokeza kuwaunga mkono.


Share To:

Post A Comment: