NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu mara baada ya kufanikiwa kuichapa Mtibwa Sugar kwa mbao 3-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yaliwekwa kimyani na mshambuliaji Fiston Mayele, Djuma Shaban pamoja na Azizi Ki ambaye alifunga idadi ya mabao kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake.

Yanga sasa iitakuwa inaongoza ligi ya NBC kwa kufanikiwa kucheza mechi nne na kujikusanyia pointi 10 akifuatiwa na Simba Sc ambaye amecheza mechi tatu na kupata alama 7 sawa na timu ya Namungo pamoja na Singida Big Star.
Share To:

Post A Comment: