Mkuu wa wilaya ya Kaliua Paul Chacha amesema halmashauri hiyo ilizalisha na kufanya mauzo ya tumbaku kilo milioni 10,842,351 hivyo kuifanya wilaya hiyo kuongoza kwa uzalishaji wa zao hilo nchini Tanzania.

Akizungumza mbele ya waziri mkuu Kasim Majaliwa Chacha amesema wastani wa bei ya kitaifa kwa zao la tumbaku ilikuwa dola 1.79 ambazo ni sawa na tsh 4174.12 kwa kilo kutokana na usimamizi uliouwekwa na uongozi wa wilaya hiyo tumbaku iliuzwa dola 1.93 ambayo ni sawa na tsh 4500.76.

Amesema kwa namna hiyo wakulima wa Kaliua wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuleta wanunuzi wa zao la tumbaku waliongeza tija.
Share To:

Post A Comment: