Waziri mkuu Kasim Majaliwa ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora kutumia pesa za mapato ya ndani kukamilisha jengo la utawala la halmashauri hiyo ambalo linajengwa kwa fedha za serikali kuu.

Majaliwa amesema muhimu kuonesha nia kwa kutenga pesa kidogo kwa ajili ya umaliziaji wa jengo hilo,Waziri mkuu ameyasema hayo katika ziara ya kikazi mkoani Tabora ambapo amesema ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo na kwamba serikali haitoacha kutoa fedha za kumalizia ujenzi huo.
Share To:

Post A Comment: