Na Imma Msumba ; Arusha

Wasindikaji wa vyakula pamoja na Wafanyabiashara wametakiwa kuwa na utaratibu unaoonesha mchanganyiko unaotumika katika bidhaa zao ili kumruhusu mlaji kufanya maamuzi kabla yakufanya manunuzi nakujiepusha na magonjwa yasiyo ambukiza yanayotokana na baadhi ya vyakula.


Mtaalamu wa Afya na Mazoezi kutoka shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyo ambukiza, Dkt. Waziri Ndonde  akizungumza jijiji Arusha wakati wa majadiliako yakufikisha elimu kwa jamii namna yakujiepusha na tabia bwete na ulaji wa vyakula usiozingatia viwango, ambaye amesema watu wengi hununua vyakula bila kuzingatia mchanganyiko uliopo nakupata athari.

Dkt. Ndonde amesema kuwa kwa sasa Wanafanya tafiti zitakazosaidia kuondokana na kasi ya kuenea kwa magonjwa yasiyo ambuliza yanayo sababishwa na matumizi ya vyakula visivyo faa.

Pia Dkt Ndonde, ameongeza kuwa namna pekee itakayo saidia kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo kisukari pamoja na magonjwa ya moyo ni pamoja na kuacha tabia bwete na kuanza kufanya mazoezi ikiwa ni njia pekee ya kupunguza athari zitokanazo na matumizi ya vyakula.

Hata hivyo Dkt Ndonde amesema ipo haja ya mamlaka zinazo simamia chakula na dawa kutunga sheria madhubiti pamoja na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyakula na dawa ikiwa ni mpango wa kusaidia Afya ya jamii.








Share To:

Post A Comment: