Na Theophilida Felician Kagera.Wakulima wa zao la vanilla kata Kagondo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya kukwama kuuza mavuno ya vanilla kutoka na ukosefu wa wanunuzi wa bei za  uhakika wa vanilla zao.Wakizungumza  baadhi ya wakulima na Blog hii mashabani mwao wamesema kuwa wameshindwa kuyauza mavuno yao kwa  wanunuzi  wachache wanaojitokeza kuyanunua kwa bei ndogo ya Shi Elfu( 30) wakati walitegemea yauzwe kuanzia japo bei ya Sh Elfu (60) nakuendelea hali iliyowapelekea kuzipaki majumbani mwao ili kuepuka kuziuza kwa bei ya maumivu  kama hiyo. Mzee Deusdedit Mwombeki ni mkulima wa mtaa wa kagondo kaifo kata hiyo ya kagondo amesema kuwa katika kuvuna kwake alivuna kilo( 47 ) akatafuta mtalaamu aliyemusaidia kuzichakata nakuzifunga  na mpaka sasa amezihifadhi nyumbani kwake akingojea kupata wanunuzi angarau wa bei zaidi ya hiyo Elfu (30)Amefafanua  kwamba awali walikuwa wakiuza vanilla  zao  katika  shilika la maendeleo ya wakulima MAYAWA na wengine ila kwa musimu huu imewawea vigumu kutokana na wao kutaka kununua kwa bei hiyo ndogo "kuna kampuni kadhaa wananifuata niwape vanilla yangu kwa bei hiyo lakini nimegoma naendelea kuhangaika huku na kule kutafuta watu wenye bei rafiki tayari  nimeishampata mtu mmoja atakuja kuichukuwa kwa Sh laki tatu (300,000) kwa kilo moja  (1) iliyokwisha chakatwa" Amesema mkulima Mwombeki. 
Licha ya changamoto ya masoko ameizungumzia pia changamoto ya uhaba wa watalaamu  mahususi wa kuwasaidia wakulima wa zao hilo kwani wanaosaidia kwa sasa  wengi wao wanakuwa hawana ujuzi zaidi wakuilifahamu vizuri zao la vanilla hivyo wanajikuta wakulima wakitumia nguvu nyingi badala ya ujuzi  katika uzalishaji.Hata hivyo ameiomba  Serikali hususani ya Mkoa  kutilia nguvu zaidi katika kulishughulikia  zao hilo lenye kiwango kikibwa cha  fedha "natamani litazamwe kama lilivyo zao la kahawa wakulima tutanufaika na Serikali itanufaika na mapato yake kama ilivyo kwa mazao mengine likiwemo zao la kahawa" Amehitimisha akisisitiza hayo mzee huyo. Mwakilishi wa wakulima wa vanilla Tarafa ya Bugabo kata ya Kishanje Halmashauri ya Bukoba Suleimani Ibrahimu amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo ameamua kuiuza vanilla yake kwa bei ya maumivu ya Sh Elfu (20) kwa kilo moja ( 1) huku wengine wakiiuza kwa Sh Elfu (15) mpaka Elfu ( 30) tofauti na yalivyokuwa mategemeo ya wakulima walio wengi hivyo naye ameiomba Serikali kama ilivyokwisha sema kuzitatua changamoto kwa zao hilo ifanye hivyo kwani wakulima wanapenda sana kulilima zao hilo japo wanaanza  kukata tamaa na ulimaji wake wakati ni zao ambalo ni la kiwango kikubwa mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika mashariki.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: