Na John Walter-Manyara

Wanakijiji wa kijiji cha Diffir kata ya Ufana wilayani Babati mkoa wa Manyara wanalazimika kuamka asubuhi mapema wakiwa na mikokoteni inayovutwa na punda na ng'ombe  kutafuta maji  umbali mrefu.

Picha mbalimbali zilitumwa kwenye mtandao wa Whatsapp na diwani wa kata hiyo Bernad Bajuta zikionesha msafara wa Mikokoteni yenye madumu na mapipa ikivutwa na Ng'ombe wakielekea kusaka maji.

Bajuta amesema aliwasiliana na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Babati (BAWASA) ambao walimweleza kuwa wanafanya ukatabati katika chanzo cha Donya ili maji yafike kijiji cha Diffir.

Kata ya Ufana ipo Katika Tarafa ya Bashnet  ukanda wa juu ambapo hakuna chanzo cha maji.

Share To:

Post A Comment: