Na Mwandishi Wetu Bungeni

SERIKALI imesema kuwa inaendelea kufanyia upembuzi yakinifu mabonde 22 yenye lengo la kufanya kilimo cha umwagiliaji  nchini.

kauli hiyo imetolewa leo bungeni  jijini Dodoma na  Naibu Waziri wa kilimo Antony Mavunde wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage.

Aidha Mwijage  alihoji  ni kwa nini Serikali isishirikishe sekta binafs katika Kilimo cha umwagiliaji ili kutimiza Ajenda 1030.

Mavunde amesema Serikali katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali katika sekta ya kilimo imeendelea kushirikiana bega kwa bega na sekta binafsi. 

"Kwa muktadha huo, katika miradi ya umwagiliaji ambayo Serikali inatekeleza kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kuishirikisha sekta binafsi katika hatua mbalimbali za miradi hiyo ili kufikia malengo ya Agenda 10/30" amesema  Mavunde.

Aidha amesema kuwa   katika kipindi Cha  mwaka 2022/2023 Serikali imepanga kukarabati na kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika eneo la hekta 95,000, ambapo jumla ya kandarasi 55 zitatolewa kwa sekta binafsi. 

"Mpaka sasa jumla ya mikataba 21 ya wakandarasi imesainiwa na Serikali

kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji" amesema Mavunde.

Share To:

Post A Comment: