Kinywaji cha viungo:
Hiki ni kinywaji chochote ambacho kimetengenezwa kwa kuwekwa viungo. Kinywaji hiki kinaweza kuwa cha moto au cha baridi. Kinywaji cha baridi kinapotengenezwa, yatumike maji yaliyochemshwa.

Chai:
Hiki ni kinywaji ambacho hutengenezwa kwa kutumia maji ya moto na majani ya chai. Wakati mwingine sukari na maziwa huongezwa. Mara nyingine watu wanapotengeneza vinywaji vya viungo huviita "chai" hata kama havina majani ya chai. Ukweli ni kwamba chai ni yale majani ya chai. Katika kijitabu hiki vinywaji vya viungo havikuitwa chai.


BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDA ZAKE
Kitunguu saumu (Garlic)
Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye
rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa.

Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni. Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani, maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi.

Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita kwa siku hasa kama vitatumika vibichi .

Tangawizi (Ginger)
Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga. Ta n g a w i z i inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa. Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au kwenye chakula.

Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu.

Iliki (Cardamom)
Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula au katika vinywaji.

Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu, kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula na huongeza hamu ya kula.

Mdalasini (Cinnamon)
Mdalasini ni kiungo kinachotokana na magome ya mmea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwa au kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini huweza kuongezwa kwe n ye chakula au katika vinywaji vilivyochemshwa au baridi.

Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu, vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hiki huongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizo katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha. Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini na tangawizi kinaweza kutuliza kikohozi.

Giligilani (Coriander)
Giligilani ni aina ya kiungo ambacho majani na mbegu zake huwez a kutumika kama kiungo katika mapishi ya vyakula mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi.

Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi
ya bakteria na fangasi.

Kotimiri (Parsley)
Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula. Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto wa tumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha. Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng' e n yo

tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa. Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji ya ziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwa katika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula.

Karafuu (Cloves)
Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungo hiki huweza kutumika peke yake au kwa kuchanganya na viungo vingine. Kiungo hiki husaidia kuleta hamu ya kula na kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni.

Vilevile karafuu husaidia kupunguza kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenye uvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa. 

Binzari (Turmeric/Yellow Root)
Binzari halisi hutokana na mizizi ya mmea wa binzari manjano ambao hufanana na ule wa tangawizi. Mizizi ya binzari huweza kukaushwa, kusagwa na kutengeneza unga wa binzari ya manjano ambao hutumika kama kiungo cha chakula. Vilevile binzari mbichi inaweza kutwangwa na kutumika kwenye

Mapishi mbalimbali. Binzari ikitumiwa katika chakula, hukifanya kuwa na rangi ya njano. Binzari inaweza kutumika kwenye mapishi ya wali au vyakula vingine vya nafaka, pia kwe n ye mchuzi au
maharagwe. Binzari husaidia katika uyeyushwaji wa chakula na pia husaidia mwili usiharibiwe na kemikali mbaya.

Ni vizuri kuwa waangalifu tunaponunua binzari ile ya unga kwani wakati mwingine wauzaji huuza binzari ambayo si binzari halisi. Binzari hii ambayo si halisi hutengenezwa kwa kutumia aina za unga wa nafaka ambao huchanganywa na rangi ya manjano na binzari kidogo.

Limau (Lemon)
Limau linaweza kutumika kama kiungo katika chakula na vinywaji kama chai au vinywaji vingine.

Limau husaidia kuboresha uyeyushwaji hasa wa protini na mafuta. Limau pia huweza kutuliza vidonda vya kooni, kikohozi, homa na kuondoa msongo.

Binzari nyembamba (Cumin seeds)
Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu za giligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali mfano; supu, mchuzi, wali, n.k.
Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza maumivu ya tumbo na hata kuharisha.

Mrehani (Basil)
Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwa kuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwaji wa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa.

Kwa vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumika kwa kusukutua.

“Calendula”
Vikonyo vya maua ya ‘‘calendula’’ vina kemikali inayozuia kukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na pia kupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatory function). Vilevile “c a l e n d u l a” hupunguza maambukizi mbalimbali katika mfumo wa chakula. ‘‘ C a l e n d u l a’’ inaweza kutumika kutibu vidonda.

Vilevile inawez akutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni.

Pilipili (Cayenne)
“Cayenne” ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamii ijulikanayo kama “capsicum”. Pilipili hizi huwa ndefu na nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina rangi nyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa na kusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwa na rangi nyekundu.

“Cayenne” huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inaweza ikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupika au wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au maji ya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi.

Shamari (Fennel)
Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzari nyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni.

Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenye chakula. Mbegu za shamari zinawez a kutumika kuandaa chai au kinywaji chochote cha moto. Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi.

Nanaa (Mint)
Nanaa ni majani ya mnanaa ambayo hutumiwa kama kiungo. Nanaa husaidia katika kuzuia hali ya mwako wa moto tumboni, kupunguza kichefuchefu, kuzuia kutapika na kuharisha. Pia huweza kupunguza maumivu ya tumbo na mkakamao wa misuli. Vilevile nanaa husaidia katika uyeyushwaji wa chakula tumboni.

Nanaa iliyooshwa vizuri kwa maji safi na salama inawez a kutafunwa. Vilevile inaweza kutumika kutengeneza kinywaji cha moto au kusukutua wakati mtu anapokuwa na vidonda kinywani

“Thyme”
‘‘T h y m e’’ inaweza kuzuia maambukizi yanayosababishwa na bakteria au fangasi. Vilevile kiungo hiki husaidia kupunguza kikohozi na kulainisha koo.

Zaidi ya hayo “thyme” husaidia ukuaji wa bakteria wazuri wanaosaidia katika uyeyushwaji wa
chakula tumboni. Inaweza kutumika kama kinywaji cha moto au kusukutua.

Meti (Methi)
Meti ni majani ya mmea uitwao kwa Kiingereza “Fenugreek”. Kwa Kiswahili inaitwa (Uwatu) Hii ni aina ya kiungo ambacho huchochea uvunjaji wa kemikali mwilini yaani umetaboli. Majani ya meti yanaweza kukaushwa na kutumika kama kiungo au kutumika yakiwa mabichi.

Vilevile mbegu za “Fenugreek” UWATU huweza kukaushwa, kusagwa na kutumika katika kutengeneza unga wa viungo yaani “curry powders”. Meti inaweza kutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na mboga za majani na vilevile katika mapishi mbalimbali ya samaki. 
Share To:

Post A Comment: