Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)Dk. James Mataragio (katikati) akizungumza leo Septemba 14, 2022  wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga katika Kijiji cha Ntondo mkoani Singida.
Meneja wa mradi huo, Gilbert Baheshe akitoa maelezo ya mradi huo.
Meneja Mkazi wa mradi huo,  Trevor  Pattern akitoa maelezo machache kuhusu mradi huo.
Meneja Mkazi wa mradi huo,  Trevor  Pattern akimuelekeza jambo Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk.James Mataragio wakati wa ukaguzi wa mradi huo.
Ukaguzi wa mradi huo ukifanyika.
Ukaguzi ukiendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)Dk. James Mataragio akisalimiana na Mzee Juma Hamisi mnufaika wa mradi huo.
Mratibu wa mradi huo,  Safiel  Msima akielezea mradi huo. Kulia ni Meneja Mawasiliano TPDC na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)Dk. James Mataragio. 
Picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa mradi huo.
Picha ya pamoja na mnufaika wa mradi huo Mzee Juma Hamisi Mwengo.
Muonekano wa eneo la mradi huo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio amewataka watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania ili kujiongezea kipato na utaalam kwani sehemu kubwa ya bomba linapita nchini Tanzania.

Mataragio  ameyasema hayo leo Septemba 14, 2022 wakati akikagua maandalizi ya ujenzi wa mradi huo uliopo eneo la Ntondo mkoani Singida ambao upo katika hatua ya kuandaa eneo zitakapo jengwa nyumba watakazokuwa wakikaa watu zaidi ya 500 watakaokuwa wakifanya kazi katika mradi huo.

Alisema eneo hilo yatakuwa yakihifadhiwa mabomba ambayo yatachomelewa Sojo na yakifika hapo yatakuwa yakisambazwa kwenye mkuza kutokea mkoani Kagera hadi Tanga na katika makambi mengine 14.

“ Mradi huu ni wa muhimu kwa nchi yetu kwani  asilimia 80 ya bomba hili lipo upande wa Tanzania hivyo nawaomba watanzania wachangamkie fursa zitakazotokana na utekelezaji wa mradi huu” alisema Mataragio.

Alisema wakati wa utekelezaji wa mradi huo mkoani hapa inakadiriwa zaidi ya ajira 500 zitapatikani ambapo aliomba wahusika wa mradi huo kutoa upendeleo wa ajira hizo kwa wananchi wa mkoa wa Singida hasa wale wanaoishi jirani. 

Alisema Serikali ilisaini Mkataba wa Msingi wa Mradi (Host Government Agreement (HGA) kati yake na Mwekezaji, Kampuni ya EACOP ambapo, kupitia Mkataba huo umeainisha baadhi ya huduma na bidhaa zitakazotolewa na Watanzania pekee ikiwemo huduma za usafirishaji, ulinzi, chakula na vinywaji, huduma za malazi na usambazaji wa mafuta kwa ajili ya magari na mitambo. 

Amezitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na shajala, bidhaa za ujenzi zinazopatikana hapa nchini, shughuli za ujenzi, huduma za mawasiliano na ukodishaji wa mitambo ya ujenzi.

Dk. Mataragio alisema kazi za fidia zimeanza kufanyika kwa maeneo yote yanayopitiwa na bomba katika sehemu zinapofanyika kazi maalum na kuwa maeneo mengine kma kule Sojo tayari wameshalipwa fidia zao na kujengewa nyumba zao baada ya kuhamishwa kupisha mradi.

Dk. Mataragio aliwataka wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa na si vinginevyo kwani uzoefu unaonesha baadhi yao wamekuwa wakishindwa hadi kufikia serikali kuwanyang’anya miradi.

Katika hatua nyingine Dk. Mataragio alikwenda  kumtembelea mnufaika wa mradi huo Mzee Juma Hamisi Mwengo ambaye alikubali kutoa eneo lake kwa ajili ya kupisha  mradi huo ambapo Serikali imemjengea nyumba ya kisasa.

Mzee Mwengo alitoashukurani zake kwa Serikalikwa kujengewa nyumba ambapo alitoa wito kwa wananchi kuiga mfano wake wa kutoa maeneo yao pale serikali inapotaka kutekeleza miradi mbalimbali.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: