Tanzania na Afrika imebarikiwa kuwa na matunda ya kila aina ambayo ni mazuri kwa matumizi ya binadamu. Matunda yanaweza kutumika kama dawa na kinga kwa maradhi mengi sana ndani ya mwili wa mwanadamu.

Basi leo nataka tusome faida ya kula matunda mbalimbali


Apple (TOFAA).

Tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa matunda ya apple yana msaada mkubwa sana kuzuia aina mbali mbali za kansa, kwani quercetin iliyopo kwenye apple ni kiondoa sumu kizuri mwilini na kinasaidia kuondoa rehemu mbaya (bad cholesteral) mwilini ambayo ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo, magonjwa kama kansa na uzito mkubwa kupita kiasi.

Matunda ya Apple yana kiwango kingi cha nguzi ambazo huitwa pectin, na tafiti zinaoneshakuwa pectin ina kazi kubwa sana ya kuondoa sumu mwilini zinazotokana na heavy metal tunazozipata kutoka kwenye mazingira tunayoishi, pia inasaidia mmeng'enyo wa chakula kwenda polepole na kufanya tumbo lako liwe limeshiba daima na kukuepusha ulaji wa mara kwa mara, pia inasaidia kurudisha ulinzi wa mfumo wa chakula ambao umeharibiwa na vyakula vibaya kama junk food.
Parachichi.

 Tunda hili nia Alkali ambalo ni tunda zuri sana kwa watu ambao wapo addicted na vyakula vyenye sukari nyingi au aina yoyote ya vyakula.


Tunda hili lina madini mengi sana ya Potasium ambayo husaidia kuhakikisha mishipa yako inasukuma damu kwa msukumo mzuri wa chini, hivyo ni tunda zui sana kwa mtu yeyote mzima kiumi na ni tunda zuri kwa watu wenye shinikizo la damu, pia huimarisha mifupa na ni chanzo kizuri sana cha protini mwilini kwa wale ambao hawatumii kabisa nyama na maziwa hii ni aina ya proteini inatakiwa kuwa chaguo lako la kwanza.Ndizi.

Ndizi ni tunda ambalo pia linaangukia kwenye kundi la matunda ya Alkali, tunda hili lina wingi wa Vitamin B ambazo husaidia kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi, msongo wa mawazo, hasira za ghafra na zisizo zuirika na wenye ugomvi kila mara.

Pia tunda hili lina vitamin C, madini ya Magesium na Potasium ambazo husaidia sana vimeng'enya chakula vifanye kazi kwa kiwango stahiki na hurudisha madini mengine.

Ni chanzo kizuri sana cha sukari mwilini mwako, hivyo badala ya kula vinywaji vilivyo ongezewa kionjo cha kemikali, rangi na sukari unaweza kutumia tunda kama ndizi kwani ina sukari asili ya kutosha ambayo haina madhara kama sukari ipatikanayo kwenye junk drinks. 

Hivyo kwa wale ambao wapo addicted na vinywaji vyenye sukari, chukua dizi, menya na saga kwenye blenda yako kunywa utafurahia afya yako na kukata kiu ya vyakula na vinywaji vya sukari.Zabibu.

Zina aina ya nyuzinyuzi mahili kabisa ambayo ni pectin, aina hii husaidia kuzuia magonjwa mbali mbali ya kisukari, kansa, vidonda vya tumbo na uzito mkubwa
Ina madini mengi ya Potasium pia na ina kiwango kingi cha Tannins ambacho kinauwezo mkubwa wa kuangamiza bakteria mwilini mwako na hivyo basi tunaita na natural antibiotics

Pia zina kiwango kingi cha madini ya manganese ambayo ni madini muhimu kwa watu wenye mifupa iliyodhoofika hasa wanawake wanaokaribia kuingia kwenye kikomo cha hedhi yani menopause na watoto wadogo matunda haya ni msaada kwao, Pia mangenese husaidia aina zingine kubwa za vyakula kama wanga, protini na mafuta kuweza kuvunjwa vunjwa na tukapata Nishati mwilini na kuimarisha miili yetu.
Share To:

Post A Comment: