Na Imma Msumba ; Arusha
Uongozi wa Chama Cha Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Tanzania
Security Industry Association{TSIA} kutoka Makao Makuu kesho septemba 15 mwaka
huu watakuwa na Mkutano na Wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi Mkoani Arusha
Mkutano unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Polisi Mess majira ya saa 3
asubuhi.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo anatarajiwa kuwa Kamanda wa
polisi Mkoani Arusha,Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini,Justine
Masejo na mada mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano huo ikiwa ni pamoja na
changamoto wanazokutana nazo wamiliki wa Kampuni za Ulinzi.
Mada nyingine ni kupanga mpango kazi wa namna ya kufanya
operesheni ya ulinzi shirikishi kati ya kampuni hizo na jeshi la Polisi ikiwa
na lengo la kuthibiti vitendo vya kihalifu na kufanya kazi hiyo kwa weledi
mkubwa.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa TSIA Mkoa wa Arusha James Rugangila
alipokuwa akiongea na vyombo vya habari Jijini Arusha na kusema kuwa chama
hicho ni walinzi shiriki katika kulinda Nchi hivyo ni wajibu wao kukutana na Polisi
ili kupanga mpango kazi wa kulinda raia na mali zao.
Post A Comment: