Na Mwandishi wetu ,Mbeya


MBUNGE wa  Jimbo la Lupa Wilayani Chunya ,Masache Kasaka amesema kuwa  uwepo  wa Mwenge wa uhuru  wilayani humo umeleta fursa za kiuchumi kwa wananchi na wafanyibiashara katika kuchochea maendeleo katika kufanya shughuli mbali mbali  ambazo huwaongezea kipato.

Kasaka amesema hayo jana` wakati  akizungumza na  mtandao huu mara baada ya kukabidhi Mwenge wa uhuru kwa  Wilaya ya Mbeya  Mjini ukitokea wilaya ya Chunya .

Mbunge huyo amesema kuwa mara nyingi Mwenge wa uhuru unapokuja unachochea maendeleo kwa wilaya ya chunya hivyo ni fursa tosha kwa kila mtu mwenye uwezo kuweza kufanya ujasiliamali wa aina mbali mbali .

“Mwenge wa uhuru ulifika Chunya Septemba nane mwaka huu na kupita miradi yote ya maendeleo  kwa kuanzia kata ya Chalangwa kuzindua Zahanati ya Itumba ambayo tayari imeanza kufanya kazi kuna baadhi ya vitu vichache vilivyoonekana vimetolewa maelekezo na kufanyiwa kazi  na mradi mwingine wa Sangambi  kuzinduliwa na wananchi wameanza kutumia maji ,maeneo mengine ni sehemu ya miundo mbinu”amesema Mbunge Masache.

Kasaka amesema kwamba mradi wa Daraja la Nselele ambalo daraja hilo kwa kipindi kirefu kulikuwa na changamoto hasa kipindi cha mvua kulikuwa na changamotio  wananchi walikuwa wanashindwa kupita na watu kadhaa walifariki kipindi cha mvua hivyo kwa ujumla Mwenge umepita vizuri hakukuwa  na shida yeyote mpaka kukabidhiwa wilaya ya Mbeya mjini .

Hata hivyo Kasaka alitaja miradi iliyozinduliwa kuwa ni minne ambapo kati hiyo , mradi mmoja  ulitembelewa  na kuwa mradi kwanza  ni Zahanati , Maji ,Daraja pamoja  na kiwanda cha kuchenjua dhahabu.

Rose Akimu ni mkazi Itumba amesema ujio wa Mwenge wa Uhuru mara nyingi wananchi walio wengi hasa wanawake hujishughulisha masuala ya ujasiliamali wa kupika chakula ambao huwapatia kipato cha kuendesha maisha yao,


“Wanawake tukipata taarifa kutoka kwa viongozi wa maeneo yetu huwa tunafurahi uwepo wa Mwenge wa uhuru maana baadhi yetu tuna vikundi ambavyo hutusaidia kufanya ujasiliamali wa pamoja siku ya mkesha wa Mwenge ,hivyo tunawaambia wanawake wenzetu ambao hawajishughulishi wafanye hivyo pindi Mwenge unapokesha kwenye maeneo yao wafanye biashara wasibweteke kusubiri kupewa fedha na waume zao “amesema Akimu.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: