Ugonjwa wa kichaa cha mbwa huenda ukaibuka katika Jiji la Arusha baada ya mifugo hiyo kuzagaa katika kila kata ya Jiji hilo na kuleta madhara kwa binadamu.

Wananchi wa Kata ya Moshono,Olerieni,Muriet,Kaloleni,Sokoni One na Sakina wamesema kuwa kama idara ya mifugo Jiji haitachukua hatua huenda ugonjwa wa Kichaa cha Umbwa ukaleta madhara makubwa kwa jamii.

Akizungumzia hali hiyo Afisa Mifugo Jiji la Arusha Dkt. Onesmo Mandike alisema kuwa taarifa za kuthibiti Mbwa katika Jiji la Arusha hawezi kuzitoa kwa waandishi wa habari na kumtaka mwandishi kwenda ofisi kujua zaidi idara hiyo inafanyaje kazi.   

Share To:

Post A Comment: