Na John Walter-Kondoa

Watu wanne wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha pikipiki mbili maarufu kama boda boda kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Pomoko kata ya Haubi wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti wa kijiji cha Pomoko, Ismail Rajabu amesema tukio hilo limetokea agosti 2 mwaka huu majira ya saa moja usiku ambapo majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma na miili ya marehemu imeshapumzishwa katika nyumba ya milele. 

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma, ACP  Martin Otieno  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema waliopoteza maisha ni wanaume wanne na majeruhi ni wawili ambao bado wapo hospitali ya wilaya ya Kondoa kwa matibabu zaidi.

Aidha amewataka madereva kuwa  makini  barabarani wanapoendesha vyombo vya moto ili kupunguza ajali zinazoepukika.


Share To:

Post A Comment: