Katika kuhakikisha wakulima wadogo wa mbogamboga Nchini wanakuza kiwango cha uzalishaji pamoja na kuongeza wigo mpana wa masoko Serikali kupitia wizara ya uwekezaji ,viwanda na Biashara imewataka wakulima kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali zilipo katika maeneo yao kwa lengo la kukuza uzalishaji pamoja na kuimarisha ushindani wa biashara ndogo na za kati katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa kitengo cha uratibu wa mradi kutoka wizara ya uwekezaji , viwanda na Biashara Rita Magere ikiwa ni wakati ufunguzi wa mafunzo ya kilimobiashara kwa wakulima wadogo wa mbogamboga na matunda katika wilaya ya Bunda na Busega yatakayofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Tarehe 15 hadi 20 August mwaka huu uliofanyika katika Ukumbi wa Killpark Hotel Mjini Bunda Mkoani Mara ambapo yameweza kufunguliwa na Mkuu wa wilaya Bunda Mhe. Joshua Nassary.  


Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wakulima hao katika kuendeleza shughuli zao za kilimo cha mbogamboga na matunda


Akieleza wakati akisoma Taarifa hiyo ya mradi wa mafunzo hayo Mkuu wa kitengo cha uratibu wa mradi kutoka wizara ya uwekezaji viwanda na Biashara Rita Magere amesema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu katika pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya Tanzania Bara na Viswani Zanzibar huku akibainisha wafadhili wa mradi huo ambao ni chombo kilichopo shirika la Biashara la Dunia , UNDP ,pamoja na srikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


“ Mafunzo haya yamelenga kuwakomboa wajasiriamali kwa maana ya kuwajengea uwezo katika uzalishaji lakini pia kupunguza umasikini kwa kutoa ajira kwa wanawake na vijana Alisema Rita Magere wakati akisoma Taarifa ya mradi huo.


Kwa upande wake Afisa kilimo kutoka Halmashauri ya mji wa Bunda Adelina Mfikwa amesema uwepo wa mafunzo hayo ni jambo jema kwa wakulima kwani wanakabiliwa na chnagamoto lukuki ikiwemo uzalishaji Duni hivyo iwapo wakulima watazingatia mafunzo haya yatakuwa na tija kubwa kwa uzalishaji ,,huku akiahidi wao kama halmashauri watashirikiana nao katika kuhakikisha wanaongeza Elimu kwa wakulima hao.


Serikali wilayani Bunda Mkoani Mara imewataka wakulima kuongeza ubunifu katika kuzalisha mbogamboga na matunda hasa kwa kutumia fursa mbalimbali zilipo wilayani humo, Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Joshua Nassary ameipongeza serikali kupitia wizara ya uwekezaji , Viwanda na Biashara kwa kuandaa mafunzo yanayolenga kuwakomboa wakulima wadogo wa mbogamboga na matunda wilayani humo huku akiwataka wakulima hao kutumia fursa hiyo ya mafunzo katika kuongeza thamani ya mazao shambani pamoja na kukuza kilimo biashara.


“ Tunahitaji wakulima mtumie fursa hii ya mafunzo haya kunufaika kwa lengo la kuongeza thamani huko mashambani na kukuza kilimo Biashara na sio kilimo peke yake , hivyo nawaachia cahnagmoto ninyi wakulima wa wilaya Bunda na wilaya Busega mtumie mafunzo haya vizuri na ukizingatia tuna fursa ya ziwa vioctoria pamoja na Nchi jirani ambayo tunaweza itumia kupata masoko asanteni na nimeyafungua rasimi mafunzo haya” Aamesema Mhe. Joshua Nassary Mkuu wa wilaya Bunda

Share To:

Post A Comment: