Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa  Caroline Nombo akizungumza katika mkutano na wadau kujadili na kutoa maoni juu ya rasimu ya sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kiunzi cha uratibu wa masuala ya ubunifu nchini.
Washiriki wa mkutano wa wadau kujadili na kutoa maoni juu ya rasimu ya sera ya sayansi, Teknolojia, na kiunzi cha utatibu wa masuala ya ubunifu nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) Mh Jerry Silaa akizungumza katika mkutano na wadau kujadili na kutoa maoni juu ya rasimu ya sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kiunzi cha uratibu wa masuala ya ubunifu nchini.

Na Janeth Raphael

BAADA yamiaka 26 serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknlojia na wadau wa elimu zaidi ya miambili wamekutana jijini dodoma ili kujadili Rasimu ya sera ya sayansi, teknolojia, ubunifu na kiunzi cha uratibu wa masuala ya ubunifu nchini.

Akizungumza katika mkutano na wadau kujadili na kutoa maoni juu ya rasimu ya sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kiunzi cha uratibu wa masuala ya ubunifu nchini naibu katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Prof. Caroline Nombo amesema Maendeleo ya nchi mbalimbali yanatokana na masuala ya Sayansi teknolojia na ubunifu huku Tanzania ikiwa ni nchi ya kwanza kwa nchi za jangwa la sahara na ya tano duniani kwa kufanya ubunifu wenye tija.

Juhudi hizo, pamoja na mambo mengine, zinajumuisha kuandaa Sera, Kanuni, Miongozo na Mikakati madhubuti na inayoendana na kasi ya mabadiliko ulimwenguni kote na kukidhi mahitaji ya nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Aidha, Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo amesema kuwa Mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii duniani kote yametokana na kutilia mkazo na kuwekeza kikamilifu katika sayansi, teknolojia na ubunifu.

"Kama ilivyo kwa nchi nyingine, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya uchumi na mhimili muhimu katika kuboresha maisha ya watu wake ndio maana tupo hapa tunazijadili na kupokea maoni ya wadau lengo ni kupata mawazo ya kuboresha zaidi sekta hii ya ubunifu,"Amesema Prof.Nombo

Prof.Nombo amesema kuwa dhamira ya kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu imekuwa sehemu ya ajenda za nchi toka miaka ya 1960, sambamba na kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Utafiti wa Sayansi (UTAFITI) mnamo mwaka 1968, na kutungwa kwa Sera ya kwanza ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (ST) ya mwaka 1985,ikifuatiwa na Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ya mwaka 1996 ambayo imetumika kwa kipindi chote.

Naye muwakilishi mkaanzi kutoka UNESCO FAITH SHAYO amesema wanaamini mapitio ya rasimu yatazingatia masuala mengine kuhusu tafiti na watafiti wa kisanyasi pamoja na kuhamasisha bunifu za ndani na kuweka taratibu ya kuzitambua na kuzikubali ikiwemo kuboreshwa ili kuendana na mazingira halisi ya watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa COSTECH Dkt AMOS Nungu amesema kuwa bunifu zote zinazo fanywa watahakikisha zinaendana na usalama wa watu huku mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) (mbunge) Jerry Slaa amesema tatizo la ajira limekua ni changamato hivyo uwekezaji kwenye bunifu za hapa nchini utakwenda kukabiliana na tatizo hilo.

Kakao hicho cha siku mbili kinachofanyima jijini dodoma kinalenga kutambua jumbe zinazofanywa na COSTECH na ubunifu kwa maendeleo ya nchi pamoja na Kutoa fursa kwa wadau wa sayansi teknolojia na ubunifu kutoa maoni yao ya uratibu wa masuala ya ubunifu.
Share To:

Post A Comment: