NA OR-TAMISEMI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ma Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema, watapeleka kwenye kila halmashauri gari moja la kubebea wagonjwa (Ambulace) pamoja na Hardtop (TOYOTA LAND CRUISER) moja huku mkoani wakipata Hardtop moja kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za afya.


Amesema, tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameshatoa shilingi Bilioni 149.5 kwa ajili ya vifaa tiba na maelekezo ni kila mkoa upate gari aina ya Hardtop moja na kila halmashauri Hardtop moja na gari la kubebea wagonjwa.


"Na mpaka sasa tuko kwenye hatua za manunuzi tukikamikisha tu mtaanza kupokea magari hayo kwenye maeneo yenu;


Mheshimiwa Bashungwa ameyasema hayo leo Agosti 10, 2022 mbele ya Raia Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wake na wananchi kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.


Amesema, Mhe.Raia amewawezesha kujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya kwenye halmashauri zetu.


"Na sasa umetupatia fedha kwa ajili ya vifaa tiba na magari, nikuhakikishie tu kuwa vifaa hivyo tutavipelela kama ulivyoelekeza,"amesema Mheshimiwa Bashungwa.


Ameongeza kuwa, "Wakazi wa Mkoa wa Njombe jiandaeni tu kupokea magari yenu tutakapokamilisha mchakato tu tutayaleta,"amesema.

Share To:

Post A Comment: