Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amewasili katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya Malkia wa Nguvu Legacy Mark 2026 iliyoandaliwa na Clouds Media Group, inayofanyika katika Serena Hotel. Leo tarehe 25 Machi 2026.
Mhe. Salome ndiye mgeni rasmi katika hafla hiyo, ambapo ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Nteghenjwa Hosseah.
Jukwaa la Malkia wa Nguvu ni mpango maalum unaolenga kuwawezesha wanawake katika nyanja za kiuchumi, kijamii na maendeleo binafsi. Kupitia jukwaa hili, wanawake hupata fursa ya kujifunza, kushirikishana uzoefu na kujenga mitandao itakayowasaidia kukua katika biashara, uongozi na maisha kwa ujumla.
Aidha, jukwaa hilo huibua mijadala ya masuala muhimu yanayowagusa wanawake na kuwapa motisha ya kujitambua, kujiamini na kutumia fursa zilizopo ili kufikia mafanikio.












Post A Comment: