Muonekano wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli likiwa katika hatua za mwisho kukamili
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo ya mchoro wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli kutoka kwa Msanifu wa Majengo Yassin Mringo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akionesha Jambo Kwenye mchoro wa jengo la halmashauri ya Bumbuli wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kukagua Uhai wa Chama na kukagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 .
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na wanachama na wakazi wa shina namba 3 tawi la Ubiri, Lushoto mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wanachama na wakazi wa shina namba 3 tawi la Ubiri, Lushoto mkoani Tanga ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama na Kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akishirikia kuapa pamoja na Wanachana wapya zaidi ya 300 wa shina namba 3 tawi la Ubiri, Lushoto mkoani Tanga ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama na Kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ametoa maelekezo ya kutaka Kiwanda cha Chai Mponde kuanza kufanya kazi ifikapo Septemba mwaka huu ili wakulima wa Chai waanze kunufaika na uwepo wa kiwanda hicho ambacho kimesubiriwa kwa muda mrefu.


Akizungumza leo mbele ya wananchi, Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amesema ameaambiwa kiwanda hiko kila siku kiko kwenye majaribio tu na hakifunguliwi, hivyo umefika wakati kuhakikisha kiwanda hicho kinafunguliwa na kuanza kufanya kazi.

“Nilikuja kwa mara ya kwanza mwaka 2013 nikiwa msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana,mimi ndio niliandika taarifa kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kuelezea umuhimu wa kiwanda hicho wakati huo. Haiwezekani sasa zaidi ya nane tunahadithia kiwanda kuzinduliwa.

“Hili jambo haliwezekani na halikubaliki , nimemsikiza Mkuu wa Mkoa, napongeza msimamo wake wa kufunguliwa hiki kiwanda , msimamo wake naunga mkono na nitamlinda kuhakikisha huo msimamo unatekelezwa , nimeambiwa wahusika wanasema majaribio rasmi yataanza mwezi wa tisa na ufunguzi uwe mwezi wa 12.

“Hivi jamani si kuna watu wamekopa mbolea, si kuna watu wameanza kukatakata chai na baada ya mwezi mmoja itaanza kuchumwa, sasa watapeleka wapi?Kiwanda kifunguliwe mwezi wa tisa na kianze kupokea chai na kuchakata , mwezi wa 12 iwe kuzinduliwa rasmi na wakati huo tunakunywa chai.Hayo ndio mambo tunayoyataka”amesema Chongolo.

Ameongeza hawawezi kuwa wanakwenda mbele wanarudi nyuma, hawawezi kuwa wanapiga maki taimu kwenye mambo ya msingi ya wananchi , Rais amewaamini na kila mmoja kwa nafasi yake atomize wajibu wake.

“Mimi nitakuwa wa mwisho kuacha mzembe akitukwamisha kwenye mambo , tutamshauri mwenye mamlaka ya kuchukua hatua ili tuachane naye tusonge mbele, wako watanzania wengi wa kumsaidia Rais kwenda mbele kwa kasi na wale wataoatukwamisha wala haitakuwa gharama kuwashusha,”amesema Chongolo.

Katika hatua nyingine, Chongolo amesema kwenye elimu bado kuna changamoto ya mtoto wa kike kwenda shule ni shida , hawapeleki mabinti shule.“Changamoto ya madarasa imekwisha wanaotakiwa kwenda shule wote wanakwenda lakini kuna mabinti hawajakwenda shule , takwimu zipo

“Ndugu zangu mtu yoyote anayemzuia mtoto kwenda shule awe wa kike na wa kiume akimzuia anafanya kosa kisheria, mtoto wa kike ana haki ya kwenda shule na kwenye huu mkoa wa Tanga imedhihirika watoto wa kike wakienda shule wanakuwa watu bora kweli kweli , si mmeona wengi , msifanye makosa ya kuwakosesha fursa hiyo.

“Waacheni wapate fursa ya elimu, siku hizi hata wanaume wote wanataka wanawake wasomi ili wasaidiane kwenye maisha, sasa msipomsomesha mnataka auolewe akiachika abakie na mateso kwasababu atakuwa hana pakwenda,tunataka mabinti waende huko lakini wakiwa msada kwa familia zao,”amesema Chongolo.

Wakati huo huo Chongolo amewaaambia wananchi hao kuwa CCM imepewa dhamana ya kuongoza nchi mwaka 2020 kwa fursa nyingine na awamu nyingine na dhamana hiyo ni ya miaka mitano mpaka 2025, kwenye kuongoza nchi ukipewa dhamana hakuna kubagua wananchi, wananchi wote ni lazima uwatumike sawasawa, uwatendee haki , uhangaike na changamoto zao sababu dhamana uliyopewa ni ya wote na sio watu wachache

“Ndio maana mimi na wenzangu tumekuja huku kuonana na wananchi kuwasilikiliza kuwatembelea, na kuangalia njia sahihi ya kutatua changamoto kwa haraka. Ndugu wananchi tuliahidi mambo mengi kwenye Ilani ya mwaka 2020 , tuliahidi kwenye maji,kwenye umeme tunaona nguzo zimepanda hadi huu.

“Umeme sio anasa ni huduma , tumeahidi kwenye barabara na barabara ya kwanza ni ya Soni mpaka Bumbuli kilometa 22 lakini haitakiwi kuchukuliwa ya Bumbuli mpaka Soni pekee inatakiwa iende Bumbuli ishuke Korogwe. Hiyo ndio barabara itakuwa imekamilika, niwahakikishie barabara hii itajengwa.”
Share To:

Post A Comment: