Jeshi la uhamiaji Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 47 raia wa Ethiopia wote wa kiume kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria,raia hao wamekamatwa eneo la Mgagao Wilaya ya Mwanga Agosti 11.2022 majira ya saa tisa usiku.


Kamishina wa uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro Edward Mwenda ameeleza kuwa wahamiaji hao wamedai kuwa walikuwa wakipita kuelekea nchini Afrika ya Kusini kutafuta maisha huku dereva akiwa ni raia wa Tanzania.


"Bado tunaendelea kufanya oparasheni zetu na kuufumua mtandao wao wa usafirishaji haramu wa binadamu,tunawashukuru wananchi wa maeneo ya mipakani kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama" ali eleza Mwenda.


Kamanda Mwenda ameeleza kuwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela na faini isiyo pungua milioni 20.


Share To:

Post A Comment: