Asila Twaha- TABORA


Timu ya Dar es Salaam kwa upande wa wanaume mpira wakikakapu  leo Agosti 11, 2022 wameanza vizuri  kwa kuwafunga goli 66 wapinzani wao Arusha mechi iliyochezwa majira saa mbili asubuhi katika viwanja vya Tabora Wavulana.


Timu ya Dar es Salaam imeonekana ikicheza kwa umahiri kwa staili ya kuwapiga chenga nyingi timu ya Arusha na kuweza kufanya vizuri wakati wote.


Mashabiki wa mchezo upande wa Dar es Salaam wameonekana  wakiwa na nyuso za furaha na bashasha kwa timu yao na kuwapa nguvu kwa kuwashangilia pale walipokuwa wanafunga na kwa upande wa timu Arusha kuzidiwa chenga na kuruhusu goli 66 kutumbukizwa katika upande wao na Arusha kuambulia goli 23.


Kwa wakati mwengine kwa upande  mpira wa wavu wasichana Dar es Salaam wameichapa seti 3 Kilimanjaro kupata seti 1 na kuifanya Dar es  Salaam kuanza vizuri kwa asubuhi ya leo  wasichana wakisema mapambano yameanza na yanaendelea kwa kuutafuta ushindi.


Kwa upande wa mratibu mpira wa wavu Somo Kimwaga amesema, timu zote zipo vizuri na timu ya Dar es salaam kuonekana  kuanza vizuri asubuhi ya leo ni uandaliwaji wa  watoto katika kufanya mazoezi ameshauri ndio mechi zimeanza  na watoto wote wanafanya vizuri kwa kucheza ameshauri walimu, viongozi kuendelea kuwapa ushirikiano watoto katika michezo yao ili wafanye  vizuri zaidi.

Share To:

Post A Comment: