Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti (Kulia) akiwa na wanufaika wa program ya ufadhili wa masomo ya kilimo ijulikano kama Kilimo Viwanda, Hillary Gilbert (Kushoto-mwisho) na Winnie Mollel, wakifungua milango kama ishara ya kuzindua dirisha jipya la mwaka 2022/2023 wa maombi ya ufadhili

Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha (Kulia) akiongea na waandishi wa habari katika halfa ya uzinduzi wa dirisha la maombi ya programu ufadhili wa masomo ya kilimo ya SBL ijulikanayo kama Kilimo Viwanda kwa mwaka 2022/2023. Kushoto ni Mark Ocitti Mkurugenzi Mtendaji wa SBL na Winnie Mollel mnufaika wa programu hiyo kutoka chou cha kilimo na mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.Wanafunzi kutoka chuo cha kilimo na mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani pwani, Emmanuel Ntandu (wa kwanza kushoto) na Shabani Sabuni, Winnie Mollel, Hillary Gilbert na Clement Abraham Mollel wakishiriki katika ufunguzi wa dirisha jipya la maombi ya programu ya ufadhili wa masomo ya kilimo ya SBL kwa mwaka 2022/2023, ijulikanayo kama Kilimo Viwanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti (Katikati) akiongea na waandishi wa habari katika halfa ya uzinduzi wa dirisha la maombi ya programu ya ufadhili wa masomo ya kilimo ya SBL ijulikanayo kama Kilimo Viwanda kwa mwaka 2022/2023. Pembeni yake kushoto ni wanufaika wa program hiyo Winnie Mollel na Hillary Gilbert (Kulia) kutoka Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo, mkoani Pwani.Ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za kuongeza mchango wa sekta ya kilimo kwenye uchumi wa nchi, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza nafasi za ufadhili wa masomo ya kilimo kwa vijana wa Kitanzania wanaotoka kwenye familia zenye kipato duni.

Ufadhili huo unaotolewa kila mwaka, Hunatolewa chini ya programu ya SBL inayojulikana kama Kilimo Viwanda ambapo wanafuika hulipiwa gharama zote za masomo na kwa kipindi chote wanachokuwa masomoni.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa dirisha la maombi kwa mwaka huu, mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema programu hiyo imekuwa ikisaidia kuunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha wataalamu wapya wa kilimo ambao ni chachu muhimu katika kuwasidia wakulima kuongeza tija katika kilimo chao.

“Leo hii tunayofuraha kusimama na kusema kuwa programu hii imeweza kuwanufaisha vijana wa kitanzania zaidi ya 200. Baadhi yao wamepata fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo kwenye viwanda vyetu. Lengo letu ni kuona kuwa programu hii inakuwa na matokea chanya kwa sekta ya kilimo na kwa vijana wanaonufaika nayo pia,” alisema

Emmanuel Ntandu ambaye ni mnufaika wa programu hiyo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani na ambaye amepata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika kiwanda cha Dar es Salaam alisema “Naishukuru sana kampuni ya SBL kwa kunipatia fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo katika kiwanda chake cha Dar es Salaam kupitia progamu ya Kilimo Viwanda. Nimejifunza mambo mengi na bado naendelea kujifunza,”

Programu ya Kilimo viwanda ilianzishwa na SBL mwaka 2019 ikilenga kusaidia kuongeza wataalamu wa kilimo kupitia kutoa ufadhili wa masomo. Wanafuika wa programu ni vijana wa Kitanzani wenye ufaulu mzuri darasani na ambao wanatokea katika familia zenye kipato duni.

Katika utekelezaji wa programu hii, SBL imeingia ubai na vyuo vinne vya ndani vinavyofundisha fani ya kilimo ambavyo hupokea wanafunzi wanaolipiwa kupitia programu hii. Vyuo hivyo ni Pamoja na Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo Pwani, Chuo cha Kilimo na Mifungo cha Kilacha kilichopo Moshi Kilimanjaro, Chupo cha Kilimo Mt. Maria Goretti kilichopo Iringa na chuo cha Kilomo Igabiro kilichopo Muleba Mkoani Kagera.

Share To:

Post A Comment: