Na John Walter-Manyara


Washindi wa kitaifa katika ukusanyaji mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbulu mji wamekabidhiwa zawadi ya kombe na cheti.


Zawadi hizo zimekabidhiwa leo na mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere wakati wa kikao kazi cha Viongozi wa serikali,siasa na wataalamu kilichofanyika mjini Babati leo Agosti 10,2022. 

Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa mwaka wa fedha 2021-2022  imeongoza kwa kupata alama 89.63 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati iliyopata alama 89.53.


Halmashauri ya Hanang wamepewa cheti na kombe kwa kuongoza ukusanyaji wa mapato kitaifa kwa Halmashauri za wilaya robo ya kwanza na ya pili 2021-2022. 

Halmashauri  zilizopewa cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri kwa kupata alama A kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani, mkoa  ni Babati Mji,Simanjiro,Hanang,Babati DC na Kiteto.

Halmashauri zilizofanya vizuri Kitaifa katika vigezo vyote saba ni Mbulu Mji nafasi ya kwanza kwa kuongoza awamu zote nne,Babati DC nafasi ya pili katika robo ya tatu kitaifa ambayo imeshika nafasi ya tatu, na Simanjiro mshindi wa pili katika robo ya nne. 

Vigezo Saba ambavyo vilizingatiwa ni kukusanya mapato ya ndani,matumizi ya mapato ya ndani katika miradi ya maendeleo,utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwenye vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu,matumizi ya fedha za marejesho ya mikopo,usimamizi wa hoja na utekelezaji wa CAG pamoja na utoaji wa mrejesho na uhabarishaji wananchi kupitia tovuti.

Share To:

Post A Comment: