Na Imma Msumba, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka viongozi
wa dini kisiasa,machinga,bodaboda na mashirika yasio ya kiserikali kuendeleza
ushirikiano wa kwenda kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi.
Mongela ameyasema hayo wakati wa Mkutano wake na wadau
mbalimbali mkoani hapa walipokutana nao kwa ajili ya kuhamasihsa zoezi la sensa
ya watu na makazi kwa mkoa wa Arusha.
Amesema kwamba zoezi la uhamasishaji wa sensa ya watu
na makazi limeenda vizuri na kupokelewa vyema na jamii hivyo anaendelea kuwasihi viongozi
wote kutoka na kwenda kuongeza hamasa kwa wananchi wanaotunzunguka
ili zoezi liweze kufanikiwa vyema.
“Kwenye madhehebu ya kiislam na mengine tutumie fursa
hii pamoja na kazi kubwa iliyofanyika tutoke na twende kuongeza hamasa,basi
tuombe kukumbushana ili tujue idadi yetu kwani kazi hii ya mwanzo ilikuwa ya matayarisho ya sensa hivyo twende kwenye kusimamia na kuweka hamasa ili zoezi hili lenyewe lifanikiwe”
Amesema kwamba zoezi la Sensa ya watu na makazi sio la
siku litaanza tarehe 23 na litaenda hadi tarehe 29 ya mwezi wa
nane,Lakini kuanzia tarehe 30 hadi tarehe 02 mwezi wa tisa ni madodoso na sensa ya jamii kimsingi wananchi watambue kuwa kwenye siku za sensa sio siku za mapumziko kazi zitaendelea kama kawaida.
Awali akiongea katika hafla hiyo ErickSongo Meijo
Laigwanan kiongozi Mkuu wa kabila la Wamasai amesema kwamba Taifa bila kufanya Sensa ni sawasawa
na mtu kutembea usiku wa manane bila kuwa na mwanga lazima uwe na mwelekeo
hivyo sensa ni dira ya maendeleo.
ErickSongo amesema kwamba sensa ni dira ya kuleta maendeleo ya
watu vijijini na mijini hivyo wanahitaji madawa kwa ajili ya mifugo,Elimu,Maji,Barabara na Hospitali sambamba na watumishi wa kada hizo bila
kuhesabiwa hatuwezi kufikia malengo ya kimaendeleo tunayoyahitajia.
Kwa Upande wake Yunis Urasa Naibu Katibu wa Shirikisho
la watu wenye Ulemavu Mkoa wa Arusha amesema kwamba wanaishukuru serikali
kuweza kuwashirikisha katika uhamasishaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi
na pia wamepokea zoezi hilo la sensa na kwani watapata takwimu sahihi za watu wenye ulemavu kwa ajili
ya maendeleo yao.
Post A Comment: