Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imeibuka mshindi wa kwanza  kwenye kipengele cha Taasisi za Elimu ya juu katika maonesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Agosti 08, 2022.

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala  Prof. Charles Lugomela  amewapongeza  wanataaluma na wafanyakazi  wa taasisi hiyo kwa ushindi huo, na kuwataka kufanya tafiti nyingi zaidi ili kuleta maendeleo hususani ya viwanda katika  jamii.

"Wito wangu kwa wanataaluma wetu wa Nelson Mandela, ni kutokubweteka na huu ushindi, bali uwe chachu kwenu kuhakikisha mnakuja na tafiti nyingi zaidi ili kuleta maendeleo kwa jamii yetu na viwanda vyetu" amesema Prof. Lugomela 

Alizidi kueleza  kuwa, Taasisi ya Nelson Mandela  ni Taasisi  inayotofautiana na taasisi nyingine kwa kuwa imejikita zaidi katika masula ya kufanya tafiti na kuja na bunifu mbalimbali zenye kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Prof. Lugomela alieleza kuwa,  tafiti na bunifu zilizowekwa katika maonesho hayo ya 28 ni za tofauti, na zimejikita katika kutatua changamoto za wakulima na wafugaji. 

Share To:

Post A Comment: