Mkurugenzi wa utetezi na maboresho- LHRC, Mwanasheria Fulgence Massawe akizungumza kwenye mkutano wa kukusanya maoni na mapendekezo ya kuboresha Rasimu ya Uchambuzi wa Sheria za vyombo vya habari ulioandaliwa na MISA TAN kwa kushirikiana na ABA ROLI

Afisa Habari na Utafiti wa MISA TAN, Bi. Neema Kasabuliro akizungumza kwenye mkutano wa kukusanya maoni na mapendekezo ya kuboresha Rasimu ya Uchambuzi wa Sheria za vyombo vya habari ulioandaliwa na MISA TAN kwa kushirikiana na ABA ROLI.

Wadau wa habari wameshiriki mkutano wa siku moja wa kukusanya maoni na mapendekezo ya kuboresha Rasimu ya Uchambuzi wa Sheria za vyombo vya habari ulioandaliwa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na taasisi ya sheria ya Marekani (ABA ROLI).

Rasimu hii iliyoandaliwa na Mtaalam Elekezi, Mwanasheria Fulgence Massawe, imechambua na kuainisha vifungu vinavyoathiri uhuru na haki ya kujieleza na kupata taarifa vya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 na Sheria ya Kupata Taarifa ya Mwaka 2016 pamoja na kupendekeza maeneo ya kuboresha.

Mkutano huo umefanyika Agosti 2, 2022 jijini Dar es Salaama ambapo wadau wamepitia, kujadili na kutoa mapendekezo ya kuboresha Rasimu kabla haijawasilishwa kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki baadaye mwezi huu ili kupata uungwaji mkono kuhimiza mabadiliko ya sheria za habari nchini Tanzania.

Wadau wakiwa kwenye mkutano wa kukusanya maoni na mapendekezo ya kuboresha Rasimu ya Uchambuzi wa Sheria za vyombo vya habari ulioandaliwa na MISA TAN kwa kushirikiana na ABA ROLI

Share To:

Post A Comment: