NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amesema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umegusa maisha ya wananchi wa Kijiji cha Kitanga Wilayani Kisarawe mkoani Pwani kwa kujenga visima vya maji safi na salama ambavyo sasa vimetatua changamoto ya maji iliyokua ikikabili Kijiji hiko .


Akizungumza na Wananchi wa Kijiji hiko, Naibu Waziri Ndejembi ameipongeza TASAF na wananchi wa Kitanga kwa ushirikiano uliowezesha kukamilika kwa visima hivyo ambavyo hivi sasa vinatoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo.


Ndejembi amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuhakikisha wanavitunza visima hivyo ili viendelee kuwa msaada kwa wananchi wa eneo hilo kwa kipindi kirefu kama Serikali ilivyokusudia.


" Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha maisha yenu na haswa kupitia Mpango wetu huu wa TASAF ndio maana tumejenga visima hivi na kutatua changamoto ya maji ambayo kwa muda mrefu imekuepo hapa Kitanga, hivyo sawa niwaombe ndugu zangu kuvitunza na kuvilinda visima hivi ili viendelee kutusaidia.


Nyinyi Wananchi wa Kitanga ndio mliokua mnapata changamoto ya maji, Serikali ikasikia kilio hiko na kupitia mradi wetu wa TASAF tumefanikisha kujenga visima hapa kwenye Kijiji chenu, hatutofurahi kusikia baada ya Miaka michache ijayo visima hivi vimeharibika kwa kukosa matunzo, niwasihi tuvilinde sana," Amesema Ndejembi.

Share To:

Post A Comment: