Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Gwau, akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo wilayani Ikungi mkoani Singida aliyoifanya juzi ambapo aliweka jiwe la msingi ujenzi wa Kituo cha Afya cha Iglanson. Gwau alitumia nafasi hiyo kumuomba Waziri Mkuu kuwasaidia wapate gari la kubebea wagonjwa hasa wajawazito.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Gwau, akizungumza katika mkutano wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kuweka jiwe la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, ambapo pia aliomba Serikali kuwasaidia chakula wananchi wa wilaya hiyo baada ya kuwepo na tishio la uhaba wa chakula kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha na kusababisha mavuno kuwa kidogo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Gwau, akiwasalimia wananchi wa Ilongero wilayani Singida wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyoifanya jana.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Gwau, mara alipofika Kijiji cha Iglanson katika ziara yake ya kikazi.
Wananchi wa Iglanson wakiwa kwenye mkutano huo.
Taswira ya mkutano huo wa Iglanson.
Wananchi wa Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo wa Waziri Mkuu.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Ikungi wakiwa kwenye mkutano.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.
Watumishi wa Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.
Wazee wa Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.


 

Dotto Mwaibale na Thobias Mwanakatwe, Singida

 

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Gwao, ametangaza kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba katika kampeni ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huu kujiunga na Bima ya Afya.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge Gwau alisema mkakati aliokuja nao Mkuu mpya wa Mkoa wa Singida,Serukamba wa kutaka kila mwananchi awe na bima ya afya ni wa kuungwa mkono.

Mheshimiwa Gwau alisema yeye binafsi alishaanza kampeni hiyo ambapo tayari ofisi yake ilishatoa Bima za Afya kwa kaya 400 zenye wanufaika 2400.

" Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ukianza hilo zoezi la kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya nitakuwa balozi wako,nichukue popote nyumba kwa nyumba tutahakikisha mkoa mzima wananchi wanapata Bima ya Afya," alisema.

Mheshimiwa Gwau alisema suala la bima ya afya ni la muhimu sana sababu afya ndio kila kitu hivyo ni sisi kama viongozi ni lazima tuhakikishe wananchi wetu wanapata bima ya afya ili kuwapunguzia gharama za matibabu.

"Nampongeza RC wetu mpya naona ni mtu mwenye maono sana na atatussidia sana wananchi wa Mkoa wa Singida tumpe ushirikiano," alisema mheshimiwa Gwau.

Aidha, Mbunge huyo alimuomba mheshimiwa Waziri Mkuu serikali iangalie uwezekano wa kuwapatia chakula cha msaada wananchi wa wilaya ya Ikungi ambao wanakabiliwa na upungufu wa chakula.

Pia katika kata ya Iglanson Mbunge Gwau aliomba serikali kutoa gari la wagonjwa katika kituo cha Afya Iglanson ambalo litakuwa linawasaidia wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: