WAENDESHA pikipiki maarufu kama bodaboda na Bajaji Manispaa ya Morogoro wamefanya maandamano ya amani lenye lengo la kuhamasisha sensa ya watu na makazi katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutambua idadi ya watanzania ili kuongeza maendeleo nchini.
Akizungumza katika tamasha hilo katibu wa kamati ya maandalizi ya tamasha la sensa Bernad Msangiya amesema tamasha lina lengo la kuhamasisha jamii kuhusu sensa na kuwaomba wananchi na watanzania wote kwa ujumla kuona umuhimu wa sensa katika nchi pia kuweka uhusiano mzuri kati ya serikali, vyombo vya Dola na wananchi ili kutambua bodaboda na bajaji ni usafiri Salam na wanapaswa kuaminiwa .
Mratibu wa sensa ya watu na makazi Manispaa ya Morogoro Frank Ugwelo amesema kuwa sensa itafanyika Kwa siku sita baada ya kuzinduliwa tareh 23 mwezi 8 Hivyo amewaomba wananchi kujiandaa kuhesabiwa na kutoa ushirikiano mzuri kwa makarani wa sensa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Abdulaziz Abood amewapongeza bodaboda na bajaji Kwa kufanya tamasha la kuhamasisha wananchi kuhesabiwa pia amewaomba kuendelea kutunza amani na kuendelea kushirikiana na serikali , vyombo vya Dola ili kutunza amani ya nchi.
Pia ameeleza kuwa sensa ina lengo la kutambua idadi ya watu , makazi ,Hali ya uchumi, jinsia , umri, ambapo itasadia serikali kufanya mipango ya kiuchumi itakayo inua uchumi wa wananchi na kuboresha huduma za kijamii.
Naye Ally machela Mkurugenz manispaa ya Morogoro amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa kwani sensa ya watu itasadia kuongeza maendeleo katika manispaa na kuwezesha serikali kuongeza huduma muhimu zitakazo saidia wananchi.
Pia amasema kama manispaa imejianda kuhesabiwa kwani hamasa zimefanyika na kuwaomba wananchi wote kushiriki katika sensa ya watu na makazi.
Hivyo katika kuazimisha tamasha lenye kauli mbiu bodaboda na bajaji usafiri Salama tuko tayari kuhesabiwa viongozi mbalimbali walishiriki ili kuunga mkono katika kuhamasisha wananchi kuhesabiwa hapo agosti 23 mwaka huu.
Post A Comment: