Na John Walter-Manyara

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Danile Abraham (40) mkazi wa kijiji cha Kitwai A wilayani Simanjiro mkoani Manyara amefariki dunia baada ya kushambuliwa na Nyati wakati akipeleka ng'ombe kunywa maji jirani na hifadhi ya taifa ya Tarangire.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Limited Mhongole amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo agosti 16 ambapo amesema limetokea agosti 9 mwaka huu kijijini hapo.

Aidha kamanda Mhongole amewataka wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za wanyama pori kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama wakali ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyama hao.
Share To:

Post A Comment: