Na John Walter-Manyara

Mkoa wa Manyara umechaguliwa kuwa mwenyeji wa siku ya maazimisho ya Idadi ya watu Duniani inayotarajiwa kufanyika Julai 20 mwaka huu wilaya ya Hanang shule ya Msingi Katesh B.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere akizungumzia siku hiyo amesema amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali kutmia fursa hiyo kuuza na kutangaza bidhaa zao.

Nyerere amesema maadhimisho hayo yatakayofanyika kwa siku tatu kwa shughuli mbalimbali kufanyika,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu Kassim Majaliwa

Siku ya idadi ya watu dunani inabebwa na kauli mbiu isemayo "Dunia ya watu Bilioni nane kuhimili wakati ujao ni fursa ya haki kwa wote, shiriki sensa kwa maendeleo endelevu".


Share To:

Post A Comment: