Articles by "Majaliwa"
Showing posts with label Majaliwa. Show all posts

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2024 amefanya ziara makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuipongeza Mamlaka hiyo kufuatia ukamataji wa dawa za kulevya zaidi ya Tani 3, zilizokamatwa Disemba, 2023.

Akizungumza na Maafisa wa DCEA, Waziri Majaliwa, amesema kuwa, Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na mamlaka hiyo katika kupambana na dawa za kulevya, huku akidai kuwa, kukamatwa kwa dawa hizo ni ushindi mkubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

‘‘Nimekuja kuona mwenyewe zile dawa mlizokamata… lakini pia kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya, mafanikio haya yanaanza kuleta sura ya kwamba Tanzania si mahali sahihi kwa kuzalisha, kusafirisha, kuuza na sio mahali pazuri kwa Matumizi ya Dawa za kulevya’’,amesema Majaliwa.

Pia amesema ameitaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya zinatokomezwa nchini, huku akiahidi kuwa, Serikali itaendelea kuiwezesha mamlaka hiyo, ili iweze kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

“Nawaomba Mamlaka muendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya zinatokomezwa nchini na sisi kama Serikali tutaendelea kuiwezesha mamlaka hii ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,”ameongeza Majaliwa.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, amemshukuru Waziri Majaliwa na serikali kwa ujumla, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka kufanikisha kazi zake.

‘‘Naomba kukushuru wewe Mhe. Waziri Mkuu kwa kuendelea kuisimamia mamlaka katika kutekeleza kazi zake vizuri chini ya maelekezo na maagizo yako, ambayo unayatoa mara kwa mara kupitia kwa wasaidizi wako na sisi kama watumishi tunahakikisha tunatekeleza maagizo yako kwa weledi na ufanisi mkubwa, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana na kuwa salama”, amesema Lyimo.

Disemba mwaka jana, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilikamata dawa za kulevya zaidi ya tani 3 katika eneo la Kibada, Dar es Salaam, dawa hizo ni aina ya Heroin na Methamphetamine, ambapo kiwango cha dawa hizo za kulevya ni kikubwa ambacho hakiwaji kukamatwa nchini tangu shughuli za udhibiti zianze kufanyika.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2024 amefanya ziara makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuipongeza Mamlaka hiyo kufuatia ukamataji wa dawa za kulevya zaidi ya Tani 3, zilizokamatwa Disemba, 2023.

Akizungumza na Maafisa wa DCEA, Waziri Majaliwa, amesema kuwa, Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na mamlaka hiyo katika kupambana na dawa za kulevya, huku akidai kuwa, kukamatwa kwa dawa hizo ni ushindi mkubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

‘‘Nimekuja kuona mwenyewe zile dawa mlizokamata... lakini pia kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya, mafanikio haya yanaanza kuleta sura ya kwamba Tanzania si mahali sahihi kwa kuzalisha, kusafirisha, kuuza na sio mahali pazuri kwa Matumizi ya Dawa za kulevya’’,amesema Majaliwa.

Pia amesema ameitaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya zinatokomezwa nchini, huku akiahidi kuwa, Serikali itaendelea kuiwezesha mamlaka hiyo, ili iweze kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

"Nawaomba Mamlaka muendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya zinatokomezwa nchini na sisi kama Serikali tutaendelea kuiwezesha mamlaka hii ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,"ameongeza Majaliwa.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, amemshukuru Waziri Majaliwa na serikali kwa ujumla, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka kufanikisha kazi zake.

‘‘Naomba kukushuru wewe Mhe. Waziri Mkuu kwa kuendelea kuisimamia mamlaka katika kutekeleza kazi zake vizuri chini ya maelekezo na maagizo yako, ambayo unayatoa mara kwa mara kupitia kwa wasaidizi wako na sisi kama watumishi tunahakikisha tunatekeleza maagizo yako kwa weledi na ufanisi mkubwa, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana na kuwa salama", amesema Lyimo.

Disemba mwaka jana, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilikamata dawa za kulevya zaidi ya tani 3 katika eneo la Kibada, Dar es Salaam, dawa hizo ni aina ya Heroin na Methamphetamine, ambapo kiwango cha dawa hizo za kulevya ni kikubwa ambacho hakiwaji kukamatwa nchini tangu shughuli za udhibiti zianze kufanyika.

 


 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali iko kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa kampasi 14 mpya za vyuo vikuu kwenye mikoa ya pembezoni isiyokuwa na vyuo vikuu. 

 

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Ruvuma, Singida, Mwanza, Kagera, Tanga, Njombe, Tabora, Manyara, Simiyu, Shinyanga, Lindi, Rukwa, na Katavi.

 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 30, 2023) wakati akizungumza na wahadhiri na wahitimu kwenye mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Iringa yaliyofanyika chuoni hapo amako pia alimwakilisha Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.

 

“Hatua hiyo ni moja ya jitihada za makusudi za Serikali za kuharakisha ukuaji wa uchumi kwenye maeneo ya pembezoni, kuongeza nafasi za elimu ya ufundi, ujuzi na stadi za maisha katika maeneo hayo ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa fursa za elimu na ajira.”

 

Akielezea uboreshaji wa miundombinu ya vyuo vikuu, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea na ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo ni vyumba vya mihadhara, maabara, nyumba za walimu na maktaba.

 

“Kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Serikali inaendelea na ujenzi wa mabweni 34; vyumba vya mihadhara na madarasa 130; kumbi za mikutano ya kisayansi 23; maabara/karakana za kufundishia 108; miundombinu ya shambani na vituo atamizi 10.

 

Amesema kukamilika kwa ujenzi huo kunatarajiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma programu za kipaumbele (STEM) kutoka wanafunzi 40,000 kwa mwaka 2020 hadi kufikia 106,000 mwaka 2026.

 

Kuhusu ombi la kujengewa bweni la wasichana litakaloitwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu amesema amelichukua na ltaenda kufanyiwa kazi Serikalini.

 

Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo aliwatunuku wahitimu 1,994 wakiwemo 108 wa shahada za uzamili wa elimu (Ualimu), Utawala na Usimamizi wa Biashara, Sanaa ya Maendeleo ya Jami na Usimamizi wa Miradi, Sayansi katika Saikolojia Nasihi, Misheni na Maendeleo ya Jamii, Sheria za Habari na Mawasiliano ya TEHAMA, na mfumo wa sheria za Jinai za Kimataifa na Haki za Binadamu.

 

Mapema, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, CPA. Lilian Badi Manara alisema wanamuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awasaidie kujenga bweni la wanachuo wa kike kwani wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa kifedha.

 

“Kutokana na changamoto ya upungufu wa kifedha, tuna upungufu wa mabeni na hasa wa kike. Na matokeo yake baadhi wanalazimika kuishi mitaani ambako wanakutana na ukatili wa kijinsia na baadhi wanalazimika kuingia kwenye ndoa za muda mfupi,” alisema.


Na John Walter-Manyara

Mkoa wa Manyara umechaguliwa kuwa mwenyeji wa siku ya maazimisho ya Idadi ya watu Duniani inayotarajiwa kufanyika Julai 20 mwaka huu wilaya ya Hanang shule ya Msingi Katesh B.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere akizungumzia siku hiyo amesema amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali kutmia fursa hiyo kuuza na kutangaza bidhaa zao.

Nyerere amesema maadhimisho hayo yatakayofanyika kwa siku tatu kwa shughuli mbalimbali kufanyika,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu Kassim Majaliwa

Siku ya idadi ya watu dunani inabebwa na kauli mbiu isemayo "Dunia ya watu Bilioni nane kuhimili wakati ujao ni fursa ya haki kwa wote, shiriki sensa kwa maendeleo endelevu".