Na,Imma Msumba Arusha 

Naibu waziri wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Omari Kipanga amewataka viongozi wa taasisi na wadau  wanaojishughulisha na utoaji wa elimu jumuishi kuendelea kushirikiana na serikali katika kujenga shule na kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa ajili ya wanafunzi na watu wenye mahitaji maalum.


Dkt.Kipanga ameyasema hayo leo wakati akizindua shule jumuishi ya mfano ya sekondari Patandi iliyopo Wilayani Arumeru ambapo amezitaka familia na wadau wa maendeleo kuendelea kuona umuhimu wa kuchangia juhudi za serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu kwenye mchakato mzima wa ujifunzaji.

Kwa Upande wake Dkt.Charles Msonde Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI ameahidi kuzitatua changamoto zilizowasilishwa

Awali akitoa taarifa za utekelezaji wa ujenzi wa shule hiyo Magreth Matonya Mkurugenzi Elimu Maalum na Numuishi Wizara ya Elimi,Sayansi na Teknolojia amesema ujenzi wa shule hiyo ni kwaajili ya kusaidia walimu tarajari na wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata elimu bora inayokidhi kiwango cha kimataifa.

Sambamba na hayo Diwani wa Kata ya Akeri Julius Mungure katika hafla hiyo ya uzinduzi ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali watanzania kupitia sekta ya elimu.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe.John Palangyo ameiomba serikali kukurabati shule zote kongwe za msingi na sekondari zilizopo katika Jimbo lake pamoja na serikali kuigeuza shule ya sekondari King'ori kuwa shule ya sekondari elimu ya juu.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: