Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH), Dkt. Amos Nungu akitoa Maelezo Wakati walipotembelea miradi ya Ubunifu na Utafiti visiwani Zanzibar kwenye Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI)

Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni COSTECH, Prod. Makenya Maboko akifafanua jambo Wakati walipotembelea miradi ya Ubunifu na Utafiti visiwani Zanzibar kwenye Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI)


Na Ahmed Mahmoud

Wajumbe wa bodi ya makamishina ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) tarehe 5 Julai, 2022 watembelea miradi ya Utafiti na Ubunifu visiwani Zanzibar. 


Miradi hiyo ni ya  utengenezaji wa nyenzo inayotokana na maganda ya miwa kwaajili ya kusafishia majitaka yanayotoka hospitalini pamoja na mradi wa kuongeza thamani ya dawa za asili na kuhifadhi mimea tiba inayotumika kutibu magonjwa yasioambukiza Zanzibar.


Miradi hiyo imefadhiliwa na COSTECH kupitia mfuko wake wa kuendeleza Sayansi Teknolojia na Ubunifu MTUSATE 


Aidha COSTECH kupitia mfuko wa MTUSATE (Mfuko wa  imewekeza kiasi cha shilingi milioni100 katika Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI) ili kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Prod. Makenya Maboko akipata Maelezo Wakati walipotembelea miradi ya Ubunifu visiwani Zanzibar kwenye Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI)
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Prod. Makenya Maboko na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt.Amos Nungu wakipata Maelezo Wakati walipotembelea miradi ya Ubunifu na Utafiti visiwani Zanzibar
Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH wakitembelea kuangalia Utafiti na Ubunifu katika Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI) iliyopo visiwani Zanzibar Jana
Kikao kikiendelea kupata maelezo ya Utafiti na Ubunifu kwenye Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI) iliyopo visiwani Zanzibar
Kikao kikiendelea kupata maelezo ya Utafiti na Ubunifu kwenye Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI) iliyopo visiwani Zanzibar
Picha ya pamoja mara baada ya kutembelea miradi ya Utafiti na Ubunifu visiwani Zanzibar inayofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI)


Pia wajumbe hao walitembelea maabara za mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar na kupata maelezo mafupi kuhusu miradi hiyo.


#costechsupportinnovationintz #Utafiti #costechtanzania

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: