Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella leo amekutana na kufanya mazungumzo  na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Regine Hess. Katika mazungumzo yao Mhe. Mongella pamoja na mambo mengine amemweleza Balozi Hess juu ya fursa za nyingi za uwekezaji zilizopo Arusha zikiwemo Utalii, Kilimo na Biashara na kuwakaribisha Wawekezaji toka Ujerumani kuja Nchini hususan Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika Sekta hizo na nyinginezo.


 Kwa upande wake Balozi Hess amemuhakikishia Mhe. Mongella kuwa Ujerumani itaendeleza ushirikiano wa kindugu uliopo baina ya Nchi hizi mbili. 


Aidha, Mkuu wa Mkoa ameikaribisha Jumuiya ya Wajerumani iliyopo Mkoani Arusha kukutana naye ili kufanya majadiliano  ya pamoja  kuzungumzia fursa zilizopo na mikakati ya kuboresha mazingira ya biashara na  uwekezaji.


Share To:

Post A Comment: