NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega amesema kuwa kuna haja ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuongezewa nguvu ili waweze kuisaidia Nchi ya Tanzania kwa kuwashika mkono watafiti na wabunifu mbalimbali ambao wanabuni bunifu zenye tija kwa Taifa.
Naibu Waziri Ulega amesema hayo leo Jumanne Julai 5, 2022 alipotembelea Banda la COSTECH katika Maonesho ya 46 Kimataifa ya Biashara Dar es salaam maarufu kama Sabasaba - Jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika banda hilo Ulega amewashauri Watanzania kutembelea Banda la COSTECH kwaajili ya kushuhudia bunifu mbalimbali zilizobuniwa na Watanzania wenzetu.
" Nimeona kazi nzuri sana zinazofanywa humu ndani nawashauri Watanzania kutembelea banda hili kujionea tafiti mbalimbali za Tanzania" amesema Mhe. Ulega.
Amefafanua kuwa watanzania kutembelea Banda la Tume hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu "Tanzania ni mahala sahihi kwa Biashara na Uwekezaji ", viwanja vya Mwl Nyerere hapa Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujifunza teknolojia mbalimbali kwa manufaa ya nchi yetu.
Josephine Sepeku kutoka Atamizi ya DTBI akimpa Maelezo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alipotembelea Banda la COSTECH katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Post A Comment: