Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akionesha upendo kwa kumnywesha maji, mgonjwa Hawa Hassan kutoka Shelui, ambaye amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida wakati

akiwaongoza Wanajumuiya wa Taasisi inayojihusisha  kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima ya Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa kwa kuwapatia msaada wa chakula na vinywaji waliolazwa Hospitali ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Eid Al-Adha ilyofanyika leo.

 Wanajumuiya wa Taasisi inayojihusisha na kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima ya  Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) wakiwa na bidhaa mbalimbali na vyakula walivyotoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid al-Adha iliyofanyika leo.

Wanajumuiya wa Taasisi inayojihusisha na kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima ya  Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) wakiwa na bidhaa mbalimbali na vyakula walivyotoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid al-Adha iliyofanyika leo.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akimfanyia dua mmoja wa wagonjwa aliyelazwa kwenye hospitali hiyo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akitoa msaada wa chakula kwa ndugu wa mgonjwa aliyelazwa kwenye hospitali hiyo.
Amirat wa Taasisi hiyo Aisha Asi akitoa msaada kwa mmoja wa wagonjwa.
Katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Ramadhani Mtipa  akimpatia chakula mmoja wa waonjwa aliyelazwa katika hospitali hiyo.
Mmoja wa mtoto kutoka Taasisi hiyo (kulia) akionesha upendo wa kumpatia maji mtoto mwenzake aliyelazwa kwenye Hospitali hiyo kwa matibabu.
Wakina mama wa JAI Mkoa wa Singida wakiwa kwenye utoaji wa msaada huo.
Amirat wa Taasisi hiyo Aisha Asi (kulia) akiwa na Mwanajumuiya hiyo.
Wanajumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa msaada huo.

Mpiga picha wa kujitolea wa Jumuiya hiyo, akitafakari jambo baada ya kuchukua matukio mbalimbali wakati wa utoaji wa msaada huo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (katikati) akiwaongoza wanajumuiya hao kwenda kutoa msaada huo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amewaongoza wanajumuiya wa Taasisi ya Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) kwa kuwapatia msaada wa chakula na vinywaji wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.

Taasisi hiyo ambayo inajihusisha  kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima imetoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid Al-Adha ilyofanyika leo.

Akizungumza kabla ya kutoa msaada huo, Sheikh Nassoro alisema jambo linalofanywa na taasisi hiyo ni jambo jema kwani limejaa ucha Mungu na kila mwanajumuiya hiyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.

"Hiki mnacho kifanya ni chema mmeacha shughuli zenu, waume zenu, watoto na marafiki badala ya kusherehekea nao sikukuu hii mmeona mje kutoa faraja kwa kuwatembelea hawa wagonjwa kwa kuwaletea chakula na vinywaji hongereni sana na dhawabu yenu mtaipata," alisema Nassoro.

Naye Katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Ramadhani Mtipa alisema kila sherehe za Eid wamekuwa wakiwatembelea wagonjwa na kuwafariji kwa kuwapa chakula, vinywaji  na vitu vingine kama sabuni na kuwa jumuiya hiyo inaendesha shughuli zake nchi nzima.

Amirat wa Taasisi hiyo Aisha Asi alisema wamekuwa wakitoka msaada wa kuwatembelea wagonjwa, yatima na wale wasio na ndugu kwa kuwapatia msaada wa chakula bila ya kubagua  dini na kuwa kazi hiyo wamekuwa wakiifanya asubuhi na jioni.  

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: