.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu wa Kijiji cha Mkumbara, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu wa Kijiji cha Mkumbara, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kushoto) akikagua mojawapo ya shamba la mkonge lililoharibiwa na tembo wakati wa ziara ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu wa Kijiji cha Mkumbara, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Basila Mwanukuzi.

Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, William Mwakilema (kushoto) na baadhi ya Watendaji na Maafisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu wa Kijiji cha Mkumbara, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoa maelekezo kuhusu namna ya kuzuia tembo kuvamia mashamba ya mkonge alipokuwa akikagua shamba la mwekezaji lililoharibiwa na tembo katika Kijiji cha Mkumbara, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo.

Mbunge wa Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mnzava akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu katika Kijiji cha Kweisewa, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo.
Mkazi wa Kijiji cha Goha, Asha Musa akielezea changamoto ya tembo wanaovamia mashamba na makazi ya watu wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu katika Kijiji cha Mkumbara, Wilaya ya Korogwe Vijijini Mkoani Tanga leo.



Serikali imejipanga kuja na mfumo maalum wa kuwavisha tembo kola zijulikanazo kama visukuma mawimbi ili kutambua mwelekeo wao kwa ajili ya kuwazuia kuingia katika makazi ya watu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) katika ziara yake ya kusikiliza changamoto za wanyama wakali na waharibifu iliyofanyika leo Kijiji cha Goha, Kwalukonge na Kweisewa, Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

“Makundi ya tembo ambayo yanaonekana kuzagaa tutayaingiza kwenye mtambo na tembo viongozi tutawafunga kola zijulikanazo kama visukuma mawimbi na tutayafuatilia yameenda wapi.” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amesema kupitia njia hiyo Askari wa Uhifadhi wataweza kuwafuatilia kwa karibu na endapo kundi lolote la tembo litakuwa na mwelekeo wa kuingia kwenye makazi ya watu, watalizuia kabla ya madhara kutokea.

Aidha, ameahidi kujenga kituo cha Askari wa Uhifadhi katika vijiji hivyo ili kurahisisha zoezi la kuzuia uharibifu unaofanywa na tembo.

Pia, amesema Serikali imejipanga kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu ambapo vijana watafundishwa mbinu mbalimbali.
Kuhusu kifuta jasho/machozi ameahidi kuwa Serikali itawalipa waathirika wote ifikapo mwezi wa nane mwaka huu.

Awali, mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Goha, Mohamed Ramadhani amesema kuwa tembo wamekuwa wakivamia mashamba kila ifikapo saa 4 usiku na hivyo kuiomba Serikali kuwapeleka Askari wa Uhifadhi ili kuwa kuwasaidia wananchi kukabiliana na adha hiyo.

“Inatakiwa kila Kijiji tuwe na watu wa TANAPA ili tutoke nao kukabiliana na tembo wakati wa usiku wanapokuwa mashambani na pia watupe elimu ya kukabiliana nao” amesema Bw. Ramadhani.

Naye, Mbunge wa Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mzava ameiomba Serikali kuangalia namna bora ya kuweka uzio ili kuzuia tembo , kujenga kituo cha askari wa wanyamapori na pia kuelimisha wananchi kuhusu mbinu za kupambana na tembo wanapovamia makazi yao.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za kusikiliza changamoto za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Share To:

Post A Comment: