Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Veronica Mwelange mara baada ya kuchaguliwa Mapema Leo kuendelea na nafasi hiyo 
Sehemu ya Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wakisimama kumpongeza Naibu Meya mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 32 Mapema Leo Jijini Arusha

Na Ahmed Mahmoud 

Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha limemchagua, Diwani wa Viti Maalum (CCM), Veronica Mwelange kuwa Naibu Meya wa Jiji hilo ambaye amepata kura zote 32 zilizopigwa na madiwani hao.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 28, 2022 katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani, Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe amesema kuwa, Naibu Meya amepita baada ya jina lake kupita bila kupingwa.

Mhe. Iranqhe amesema kuwa, Veronica amefanikiwa kutetea nafasi yake baada ya kuongoza nafasi hiyo tangu mwaka 2020.

Kwa upande wake Naibu Meya huyo amesema kuwa kama ilivyo mwaka mpya wa fedha mambo yawe mapya huku akiwataka madiwani kuunganisha nguvu kujenga halmashauri hiyo.

"Mwaka uliopita yawezekana wengine tulikuwa wageni ila tumejifunza mengi na sasa tunaenda kuijenga halmashauri yetu na kuhakikisha tunaongeza mapato na kuwa mfano bora wa kuigwa."amesema Naibu Meya.

Amesema kuwa siri ya mafanikio ya kupeta mara ya pili ni kutokuwa na makundi wala makandokando katika uongozi wake ambapo amesema atahakikisha anasimamia kwa uaminifu shughuli mbalimbali ndani ya jiji hilo. 

Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ikiwemo elimu, Afya na uchumi, Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita amesema kuwa, amechaguliwa na madiwani hao baada ya kuwa na imani naye na atahakikisha anaisimamia  kamati hiyo vizuri na kwa vitendo kuhakikisha wanaboresha huduma hizo ipasavyo.

Diwani wa Kata ya Kati Abdulrasul Toja akipiga kura kwenye Baraza la Mwaka lililofanyika Mapema Leo Jijini Arusha 
Madiwani wakiwa katika shughuli za uchaguzi wa Naibu Meya Mapema Leo Jijini Arusha 

Naibu Meya Veronica Mwelange wakiwa washukuru Madiwani mara baada ya kuchaguliwa kuendelea na nafasi hiyo kwa kipindi Cha pili Mapema Leo Jijini Arusha

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: