Mwenyekiti wa bodi chuo cha Usanifu wa madini Arusha TGC Dkt.George Mafulu ameishukuru serikali kwa kuwapatia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 7 katika mwaka mpya wa fedha wa fedha kwa ajili ya upanuzi ya miundombinu ya kituo.


Akizungumza nasi Dkt.Mafulu amesema kupitia kikao cha bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni wameweza kujadili mambo mbalimbali ikiwemo  namna bora ya kuendeleza kituo hicho na jinsi ya kuendeleza upanuzi wa miundombinu ya kituo.


Aidha amesema ili kuweza kusimamia vyema menejimenti ya kituo hicho iweze kitekeleza jukumu la usimamizi wa miundombinu wamekuwa na ziara za mafunzo za kuwajengea uwezo.


"Tumeweza kutembelea chuo cha ufundi Arusha na tumeonea jinsi ambavyo wana miradi mingi ya upanuzi wa miundombinu na pia tumetembelea chuo cha Uhasibu Arusha nao wametupa uzoefu wao katika kutekeleza miradi ya miundombinu."Alisema Dkt.Mafulu


Ameongeza kuwa uzoefu ambao wameupata katika vyuo walivyotembelea umewapa picha nzima ya namna ambavyo tutasimamia kituo katika kuhakikisha ipanuzi wa miundombinu yake.


Dkt.Mafulu ameongeza kuwa kituo cha TGC kina mchango mkubwa katika kutoa mafunzo kwa njia ya vitendo na kinawasaidia watu kupata ujuzi ambao unawapeleka moja kwa moja sokoni na kuweza kukabiliana na changamoto za ajira.


Share To:

Post A Comment: