Waziri wa Ardhi na maendeleo ya makazi Mhe.Angelina Mabula amepiga marufuku matumizi ya aina yoyote katika Shamba la Stain lililokuwa chini ya uwangalizi na Halmashauri ya Monduli.


Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Monduli katika kikao kifupi kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli.


Mhe.Mabula amesema Halmashauri ya Monduli haina tena mamlaka ya kusimamia Shamba hilo bali litakuwa chini ya Mamlaka ya Wanyapori Tanzania (TAWA) kwa uwangalizi zaidi.


Halmashauri ya Monduli imenyang'anywa uwangalizi huo baada ya kuweka mwekezaji kinyume cha sheria za usimamizi wa Ardhi kwani walitakiwa kuomba kibari kutoka kwa mmiliki ambae ni msajili wa hazina.


Amesema Halmashauri ilikiuka sheria kwa kubadili jina la Shamba  ilingali jina la Shamba lilikuwepo,pia mkataba walioingia na mwekezaji haukuwa wazi sana kuonesha niwa miaka mingapi.


Kutokana na ukiukwaji huo wa taratibu na sheria Wizari ya Ardhi imeondoa mamlaka ya uwangalizi wa Shamba hilo kutoka kwa Halmashauri ya Monduli na kupatia TAWA.


Nae, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amesema Shamba la Stain lipo katika  mapito ya wanyama na ni eneo la ikolojia ya hifadhi ya Manyara na Tarangire hivyo wao kama Wizara wana jukumu la kuliangalia kwani ni Maliasili ya nchi.


Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe.Festo Ndugange amewataka viongozi wa Halmashauri ya Monduli kuwa na subira wakati Serikali kuu ikiendelea kuweka  taratibu za namna ya kulisimamia na kuliendeleza Shamba hilo.


Dkt. Ndugange amesema Serikali ni moja inayofanya kazi kwa ushirikiano kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi


Shamba la Stain lina ukubwa wa ekari 15,163 likiwa linajumuisha mshamba madogo 3 Amani, Lente na Londoles ambapo katika Shamba la Amani ekari 3000 zilimegwa na Halmashauri ya Monduli kati yake ekari 1500 walipewa wanakijiji kwa ajili ya matumizi yao na ekari 1500 Halmashauri ilimpa mwekezaji  EBN hunting Safari Kampani.


Shamba la Stain lilifutwa umiliki wake mnamo mwaka 2005 na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania marehemu Benjamin William Mkapa kutoka kwa mwekezaji  bwana Herman Stain na Julai 2018 Serikali ilichukua umiliki wake na Halmashauri ya Monduli ilikasimiwa mamlaka ya kuwa msimamizi wa Shamba hilo.

Share To:

Post A Comment: