Na Ahmed Mahmoud


Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),Mizengo Peter Pinda Leo Julai 4, 2022 ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na kutoa Kongole kwa Tume hiyo kuendelea kuibua vijana wenye bunifu katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (TANTRADE) maarufu kama Sabasaba – Tanzania Jijini Dar es salaam.


Amesema bunifu zilizopo kwenye banda la COSTECH zimempa matumaini makubwa huku akisisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Tume hiyo kuwashawishi viongozi wa Wizara husika kutembelea banda hilo ili kujionea bunifu na Teknolojia rahisi kwa kuwasikiliza wabunifu hao kwasababu bunifu zao zinaweza kuleta tija katika maendeleo ya Nchi.


Amesema kuwa amevutiwa na bunifu ya kijana aliyebuni teknolojia rahisi ya kumsaidia mkulima mdogo kwa kumtambua na kumsajili katika eneo lake la shamba , kutambua aina ya mazao anayotumia ili kuweka mazingira wezeshi ya kumsaidia mkulima kutambulika kirahisi zaidi. 


Pinda ameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuendelea kuwashika mkono wabunifu hapa nchini na kusisitiza kuwa bunifu hizo zisiishie njiani bali ziendelezwe na kuleta tija kwa kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: