Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameunda kamati ambayo itapitia mfumo wa uzalishaji pamoja na mchakato wa ugavi unaotumika katika tasnia ya Sukari Wilayani Kilombero ili kuweza kupatikana mwarobaini wa changamoto zilizopo ndani ya tasnia hiyo.


Waziri Bashe ameunda kamati hiyo ambayo itaoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bwana Gelard Mweli, Julai 17, 2022 wakati wa mkutano wake na Wakulima wa miwa wa mashamba ya Kilombero.

Aidha, Waziri Bashe ametoa agizo kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika pamoja na Kampuni ya Sukari ya Kilombero kufanya usanifu wa kina ili serikali itengeze miuondombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya wakulima wa miwa.

Ameongeza kuwa Serikali itaanzisha Kitalu cha kuzalisha mbegu za miwa wilayani Kilombero ili kuongeza uzalishaji katika tasnia hiyo ya sukari.

Vilevile, ametoa wito kwa Wakulima, Viongozi wa Serikali, Ushirika na Sekta Binafsi kuwa na mshikamano ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya sukari.

Aidha amekemea vitendo visivyo vya uadilifu vinavyofanywa na baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika na kusababisha migogoro.

“Hakuna Kiongozi wa Ushirika atakayekula hela ya Mkulima akabaki salama." Amesisitiza Waziri Bashe.


Share To:

Post A Comment: